Wakati toka juzi kukienea taarifa kuwa tayari umoja wa katiba ukawa umemaliza
kazi ya kugawana majimbo ya uchaguzi katika mkoa wa Dar es salaam na kuwa
tayari kila mtu ameshapata jimbo lake,chama cha democrasia na maendeleo chadema
mkoa wa temeke leo kimekanusha maneno yaliyoenezwa kuwa tayari jimbo hilo
wameshapewa chama cha CUF .
Akizugumza na wanahabari leo mwenyekiti mh BERNARD
MWAKYEMBE kwa niaba ya kamati tendaji ya jimbo hilo amesema kuwa jimbo
haligawiwi kama pipi kwani wanaamini kuwa viongozi wa UKAWA watatoa mwongozo ambaop
kila chama kitatoa mgombea na baada ya hapo kutakuwa na kura ya maoni pamoja na
kuchagua mgombea na baada ya hapo anayekubalika napande zote atapewa nafasi ya
kugombea katika jimbo hilo.amesema kuwa habari ambazo zimeenezwa na magazeti
leo kuwa jimbo hilo limepewa CUF ni uzushi na uhuni mkubwa
No comments:
Post a Comment