Juu Mheshimiwa Zitto Kabwe na wabunge wengine wakitoka Bungeni mjini Dodoma leo. Chini akiwa na Mbunge wa Ludewa Mhe. Deo Filikunjombe (kuhoto) na Mbunge mwingine |
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Zuberi Kabwe (pichani) usiku huu ametangaza rasmi Bungeni Dodoma kuachia kiti hicho alichokipata kupitia CHADEMA.
Mhe. Kabwe ametangaza kung'atuka nafasi hiyo baada ya Mwenyekiti wa Bunge Mhe Mussa Hassan Zungu Kumruhusu kutoa kauli binafsi mara baada ya wabunge kumaliza kupitia vifungu vya sheria ya Maafa ambayo hata hivyo haikupitishwa kwa kutotimia akidi ya wabunge ambao nusu yao hawakuwepo ukumbini.
Mhe Zungu alimtakia kila la heri Mbunge huyo machachari ambaye amesema ameamua kuachia ngazi baada ya chama chake kumfukuza. Hata hivyo alimalizia kwa kusema kwamba Mungu akipenda atakuwa nao tena mwezi Novemba mwaka huu. Hakufafanua. Video ya tamko lake hilo hii hapa...
Mhe.Zitto Kabwe akiongea na waandishi wa Habari usiku huu mara baada ya Kuwaaga Wabunge Baada ya kuwasomea barua aliyomwandikia Mhe.Spika ya Kung'atuka Ubunge baada ya kuvuliwa Uanachama na chama chake cha CHADEMA
No comments:
Post a Comment