Friday, March 27, 2015

KUHUSU KIINGILIO CHA TAIFA STARS NA MALAWI,SOMA HAPA


KUIONA STARS, THE FLAMES  5,000/


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, limetangza viingilio vya mchezo wa siku ya jumapili kati ya Taifa Stars (Tanzania) dhidi ya The Flames (Malawi) utakaochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuwa ni tsh. 5,000 mzunguko na tsh. 12,000 kwa jukwa kuu.

Kuelekea mchezo huo wa jumapili kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa CCM Kirumba huku wachezaji wake wote wakiwa na ari na morali ya juu tayari kwa kuwakabili the Flames.

Taifa Stars iliyo chini ya kocha mkuu Mart Nooij iliwasili jijini Mwanza siku ya jumanne na kufikia katika hoteli ya La Kairo iliyopo eneo la Kirumba,
ikiwa na kikosi  kamili kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa uliopo kwenye kalenda ya FIFA.


Maandalizi ya mchezo kwa upande wa Taifa Stars yamekamilika, timu imekua ikifanya mazoezi katika uwanja wa CCM Kirumba ambao ndio uwanja utakaotumika kwa mchezo.

Wachezaji waliopo jijini Mwanza ni , Aishi Manula, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Salim Mbonde, Haji Makame, Hassan Isihaka na Abdi Banda.

Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Haroun Chanongo, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Frank Domayo, Said Ndemla, John Bocco, Juma Luizio, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.


MALAWI YAWASILI MWANZA
Timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) tayari imewasili leo jijini Mwanza majira ya saa sita mchana, ikiwa na kikosi chake kamili kwa ajili ya mchezo dhidi ya Taifa Stars siku ya jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Malawi imewasili ikiwa na kikosi chake kamili cha wachezaji 18 na kufikia katika hotel ya JB Belimonte, wakiwemo wachezaji saba wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.

Wachezaji wa kimataifa waliowasili ni nahodha Joseph Kamwendo (TP Mazembe -Congo DR), Chimango Kayira (Costal de Soul - Msumbiji), Frank Banda (HBC Songo - Msumbiji), Esau Kanyenda (Polokwane City - Afrika Kusini),  Harry Nyirenda (Black Leopards - Afrika Kusini), Limbikani Mzava (Celtic - Afrika Kusini) Gerald Phiri (Caps United - Zimbambwe)

Wegine ni McDonald Harawa (Hoyale FC), Richard Chipuwa (Wanderers), Lucky Malata (Silver), John Lanjesi (Civo), Francis Mulimbika (Wanderers), John Banda (Blue Eagle), Earnest Tambwe (Surestream) , Micium Mhone (Blue Eagle), Chikoti Chiriwa (Red Lions), Peter Wadabwa (Silver) na Amos Khamula(Support Ballaton).

Mkuu wa msafara ni Alexander Waya, Kocha mkuu Young Chimodzi, kocha msaidizi Jack Chamangwana, kocha wa makipa Pillip Nyasulu, Daktari wa timu Levison Mwale, Meneja wa timu Frank Ndawa na Afisa Habari James Sangala.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Malawi kinatarajiwa kufanya mazoezi leo saa 10 jioni katika uwanja wa CCM Kirumba, huku siku ya jumamosi wakipata nafasi ya kufanya mazoezi tena kwenye uwanja huo wa mchezo.

Kesho jumamosi saa 5 kamili asubuhi kutafanyika mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya La Kairo iliyopo Kirumba jijini Mwanza, kocha wa Stars Mart Nooij na kocha wa The Flames Young Chimodzi wataongelea maandilizi ya mchezo wao wa siku  ya jumapili.

No comments: