ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA AJISALIMISHA POLISI KWA
MKUU WA UPELELEZI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limeanza kumhoji Askofu JOSEPHAT
GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima baada ya kujisalimisha kama alivyotakiwa kufanya
hivyo na Kamishana wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Askofu Gwajima alifika kituo kikuu cha Polisi saa nane na dakika kumi
na tano mchana wa tarehe 27/03/2015. Mara baada ya kufika kituoni hapo
alielekezwa kwenda kumuona Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam
SACP Constantine Masawe ambaye alikuwa akisubiri kufika kwake.
Tuhuma zinazomkabili Askofu Gwajima ni pamoja na kumkashfu na kumtukana
hadharani Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo
Taratibu za mahojiano zimekwishaanza kwa mujibu wa sheria na mtuhumiwa
atapewa haki zote anazostahili kama vile kuwa na ndugu yake wa karibu, rafiki
yake anayemwamini au wakili wake.
Kama ilivyo kawaida utakusanywa ushahidi kutoka pande zote za shauri
hilo ili kubaini ukweli wa jinsi tukio hilo lilivyotokea na athari zake.
Baada ya hapo hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja
na kupata maoni ya kitaalamu na ya kisheria ili kuhakikisha kwamba haki
inatendeka. Ili ufanisi upatikane katika upelelezi wa shauri hili, ni muhimu
kupata ushirikiano kutoka kwa kila atakayetakiwa kulisaidia Jeshi la Polisi
kukamilisha haraka upelelezi wa shauri hili ambalo sasa limepata mvuto mkubwa
katika jamii.
HAPA SAUTI YAKE AKIZUNGUZIA KILICHOTOKEA
No comments:
Post a Comment