Katibu wa msikiti huo ABDALAH MOHAMED akizungumza na wanahabari leo nje kidogo ya hafla hiyo ya kuwapongeza baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana |
Uongozi wa shule ya seminary ya mivumoni iliyopo
jijini Dar es salaam leo umefanya shughuli maalum ya kuwapongeza wanafunzi wake
waliohitimu masomo ya kidato cha nne mwaka jana baada kufanya vizuri na
kuitangaza vizuri shule yao.
Shule ya mivumoni ambayo ilianza mwaka 2006 ikiwa na
wanafunzi 108 hivi sasa ina wanafunzi 460 ambapo katika historia yake shule
hiyo haijawahi kutoa mwanafuzni aliyepata daraja sifuri tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumza na mtandao huu wakati wa hafla hiyo
katibu wa shule hiyoABDALAH MOHAMED amesema kuwa shule hiyo inajivunia baada ya
kufanikiwa kutoa wanafunzi wawili bora katika kumi bora kitaifa kwa miaka
miwili ambapo ilifanya hivyo mwaka 2009 na 2013.
Amesema kuwa kwa mitihani ya kitaifa shule hiyo
imekuwa katika kumi bora katika mkoa wa Dar es salaam kwa miaka yote sita na
kitaifa imekuwa katika shule hamsini bora na mwaka 2013 shule hiyo imepata
cheti cha ubora chini ya B.R.N na mkanda wa kijani wenmye ishara ya kuwa ni
shule bora.
Mwanafunzi YASINI RASHID ambaye pia ni mmoja kati ya wanafuynzi waliofanya vizuri katika shule hiyo akielezea siri ya mafaniko yake |
Pamoja na shule hiyo kupata matatizo ya kuungua na
moto mnamo mwaka 2014 na kupotelewa na majengo pamoja na thamani mbalimbali za
kufundishia bado shule hiyo imefanya maajabu katika mitihani ya nkidato cha nne
mwaka huo huo baada ya kupata daraja la kwanza na lapili pekee huku kukiwa
nhakuna daraja la tatu na kuendelea jambo ambalo uongozi wa shule hiyo umeliita
ni jambo la kupongezwa kwani ni juitihada kubwa sana hadi kufikia hapo.
No comments:
Post a Comment