Friday, March 20, 2015

MREMBO DORIS MOLLEL AZINDUA FOUNDATION YAKE JIJINI DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Thabit Kombo akimpongeza Mwenyekiti wa Mfuko huo,Doris Mollel kwa kuona jukumu la kusaidia jamii katika kuokoa maisha ya watoto njiti.
Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Thabit Kombo akizungumza wakati wa hafla ya kutambulisha Mfuko wa Doris Mollel,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es salaam.


Mwenyekiti wa Mfuko huo,Doris Mollel akizungumza na wageni waalikwa waliofika kwenye hafla ya kutambulisha Mfuko wa Doris Mollel,uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Thabit Kombo (pili kushoto),Balozi Mwanaid Maajar (kulia),Mwenyekiti wa Mfuko huo,Doris Mollel (katikati) pamoja na wadau wengine wa Mfuko huo wakishiriki kwa pamoja kukata keki,kuashiria uzinduzi rasmi wa Mfuko wa Doris Mollel,uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Wageni waalikwa katika hafla ya kutambulisha Mfuko wa Doris Mollel,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja na baadhi ya wadau waliohudhulia hafla hiyo.
Kutoka kulia ni HEENA ambaye ni mmoja kati ya washirika wakubwa wa mfuko huo, wakiwa wameshikana mikono na muanzilishi wa mfuko huo miss DORIS MOLLEL pamoja meneja wa mfuko huo RAHAB MBISE mara baada ya kuzindualiwa kwa mfuko huo jijini Dar es samaam

Meneja wa mfuko huo RAHAB MBISE akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jjini Dar es salaam
Mrembo wa singida aliyeshika nafasi ya tatu katika mashindano ya miss tanzania mwaka wa 2014 DORIS MOLEL leo amezindua rasmi rasmi DORIS MOLEL foundation ambayo ni mahususi kwa ajili ya kusaidia watoto ambao wamekuwa wanazaliwa wakiwa bado hawajatimia NJITI ambapo amewataka watu mbalimbali kujitokeza kumpa saport katika shighuli hiyo.

Uzinduzi huo ambao umefanyika leo jijini dare s salaam na kuhudhuriwa na viongozi pamoja na wadau wanaohusika katika kuwasaidia watoto hao  wengi wamepongeza jitihada zinazoonyeshwa na mrembo huyo kwani watoto wanaozaliwa wakiwa na tatizo hilo wamekuwa wakusahaulika sana nchini tanzania jambo ambalo limetajwa kuwaadhiri watoto hao pamoja na wazazi wao.

Mrembo DORIS ambaye nayeye ni mmoja  kati ya watu walioadhirika na tatizo hilo alizaliwa akiwa njiti akizungumza katika uzinduzi huo amesema kuwa ameamua kuwasaidia watoto na wazazi  wenye matatizo hayo baada ya yeye kupitia katika kipindi kama hicho ambapo amesema kinahitaji msaada mkubwa kutoka kwa watu wa karibu.

“Mimi nilizaliwa nikiwa njiti nilikuwa sijafikisha uzito halali wa kuzaliwa lakini nilizaliwa na mama akanisaidia hadi leo hii mnaniona hapa ni miss Tanzania na ni mtu nayekubalika na jamii,hivyo nimeona kuna haja ya kuwasaidia watoto kama mimi ambao wamezaliwa hivyo ili waweze kukua na afya njema na baadaye kutimiza malengo ya maisha yao”alisema mrembo huyo.

Amesema kuwa baada ya kuchaguliwa ,kuwa mrembo namba tatu wa Tanzania alifikiria kitu cha kufanya ili arudishe shukrani kwa watanzania na baada ya kutembea katika maeneo mbalimbali aligundua kuwa watoto wanaokumbwa na matatizo hayo bado wamekuwa hawapewi kipaumbele katika kusaidiwa jambo ambalo limemsukuma yeye kuanza kufanya mchakato huo.

Aidha amesema kuwa ipo haja ya serikali pamoja na wadau mbalimbali kuunga mkono jitihada hizo kwa lengo la kuokoa kizazi kikubwa ambacho kinazaliwa na matatizo kama hayo ambapo kwa takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watoto laki mbili wanazaliwa wakiwa njiti kwa mwaka nchini Tanzania.

Uzinduzi huo ulienda sambamba na uchangiaji wa fuko huo kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao ambapo watu mbalimbali walijitoa kuchangia mfuko huo na kuwaomba watanzania wengine kuendelea kumsaidia mrembo huyo kuhakikisha kuwa anatimiza lengo lake.

Baadhi ya watu waliojitokeza kumpa nguvu katika shughuli hiyo leo ni pamoja na muandaaji wa mashindani ya miss tanzania ambapo ndiko mrembo huyo alikotokea bwana hashimu lundenga,mwenyekiti mstaafu wa bodi ya usafiri dare s salaam UDA mzee iddi samba,Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Thabit Kombo pamoja na viongozi mbalimbali kutoka bara na Zanzibar.

No comments: