Picha na maktaba |
Watu 35 walifariki dunia papo hapo na wengine watatu wakiwa hospitali ya wilaya ya Kahama kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo na mawe yanayodaiwa kuwa na ukubwa mithili ya ndoo ndogo ya lita kumi katika kijiji na Kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga usiku wa kuamkia leo.
Malunde1 blog imeambiwa kuwa mvua hiyo imenyesha kwa muda wa takribani dakika 30,imeua pia mifugo wakiwemo ng’ombe na mbuzi na kuharibu vibaya mimea.
Afisa mtendaji wa kata ya Mwakata Mahega Mwelemi ameiambia Malunde1 blog kuwa maeneo yaliyoathirika kuwa ni cha Mwakata,Nhumbi na Magung’humwa.
Mwelemi amesema watu wengi wamefariki kwa kuangukiwa na nyumba zao,kuzidiwa na maji pamoja kupigwa mawe ya mvua ambayo hadi leo asubuhi yalikuwa yanaonekana kijijini hapo.
Mwelemi amesema watu wengi wamefariki kwa kuangukiwa na nyumba zao,kuzidiwa na maji pamoja kupigwa mawe ya mvua ambayo hadi leo asubuhi yalikuwa yanaonekana kijijini hapo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya aliyefika eneo la tukio bado wanafanya ukaguzi katika kila kaya kubaini idadi ya watu waliofariki dunia,kujeruhiwa na idadi ya mifugo iliyokufa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema watu waliofariki dunia ni 38,majeruhi 59 wamepelekwa hospitali na kuongeza kuwa idadi ya vifo na majeruhi inaweza kuongezeka.
Kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Shinyanga Elisa Mugisha amesema baada ya kupata taarifa kuwepo kwa tukio hilo walifika katika eneo la tukio na kuwakimbiza hospitali majeruhi na shughuli ya uokoaji inaendelea.
TAARIFA HII KWA MUJIBU WA MALUNDE1 BLOG
No comments:
Post a Comment