Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda
amesema kuwa wilaya ya Kinondoni inakabiliwa na changamoto migogoro ya
ardhi ambayo inatakiwa kila mtu ambaye amenyimwa haki ya ardhi watapata
kutokana na utaratibu uliopo.
Makonda
aliyasema hayo hivi karibuni wakati ziara ya kutembelea wilaya hiyo,
Makonda alisema asili ya migogoro hii inatokana hasa na mgongano wa
uhalali wa umiliki pamoja na uvamizi wa maeneo ya wazi yaliyotengwa maalumu kwa
shughuli za jamii ni changamoto ya muda mrefu na natambua juhudi nyingi
zilizofanyika katika kutatua.
Makonda
alisema moja ya mkakati wangu ni kufanya utatuzi unaohusisha taasisi zote
muhimu ili kufupisha mlolongo unaowapotezea muda walioko kwenye migogoro na
kuhakikisha mwenye haki anapewa haki yake bila kuyumbishwa.
Alisema
anatenga siku moja ambayo ni ya Ijumaa kuwa siku maalumu ya kukutana na
wananchi na kusikiliza matatizo yanayohusiana na Ardhi na utaratibu huu utaanza
machi 6 mwaka huu na zoezi la uandikishaji kwa wale wanaohitaji kusikilizwa
matatizo yao utaanza majira ya saa 3.
Makonda
alisema Ili kupata ufumbuzi usio na shaka kamati ndogo itakayohusika katika
kushughulikia matatizo hayo itaundwa na Katibu tawala wilaya (DAS) akiwa
ni katibu, Mwanasheria wa Manispaa, Afisa Mipango miji, Aidha alisema
ili kufanya zoezi hili liwe na ufanisi na mafanikio ningeomba wananchi wafuate
utaratibu kuanzia ngazi za watendaji wa chini kabla ya kufikisha kila muhusika
ahakikishe amekuja na vielelezo vyote halali vinavyoweza kutumika katika
kufikia uamuzi
|
No comments:
Post a Comment