Mheshimiwa Mbowe akiendesha baiskeli baada ya kuzindua kampeni ya Shahada mkononi na kukabidhi baiskeli kwa viongozi wa kata watakazozitumia katika kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura Hapa ni katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Nguzo Nane mjini Shinyanga ambako jioni ya leo mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amefanya mkutano mkubwa wa hadhara,ambapo maelfu ya wakazi wa Shinyanga wamehudhuria.Mambo mbalimbali yamezungumziwa katika mkutano huo likiwemo suala la katiba inayopendekezwa,daftari la wapiga kura,mauaji ya albino,rasilimali za nchi na mambo kadha wa kadha yanayohusu mstakabali wa taifa la Tanzania.Pamoja na hayo CHADEMA wamezindua Oparesheni Shahada Mkononi,Delete CCM-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga |
No comments:
Post a Comment