Wanafunzi pamoja na wanajumuiya wa chuo kikuu huria nchini Tanzania tawi la mkoa wa Temeke
wamemuaga rasmi aliyekua makamu mkuu wa chuo hicho profesa TOLLY MBWETE ambaye amemaliza kipindi chake cha kuwa katika nafasi hiyo kisheria ambapo ni miaka
kumi ya utumishi wa umma.
Profesa TOLLY MBWETE amewaaga rasmi leo wanajumuiya wa chuo hicho
kikuu huria cha Tanzania tawi la Temeke kufuatia
kuteuliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyuo vikuu barani Afrika. ambapo
pamoja na mambo mengine ameonyesha kuwashuku wanafunzi pamoja na wafanya kazi
wote wa chuo hicho waliokuwa naye pamoja katika kipindi chote cha utumishi
wake.
Biongozi wa watu wenye ulemavu tanzania akimshiukuru profesa MBWETE kwa msaada ambao chuo chake kimekuwa kikiutoa kwa watu wenye ulemavu tanzania |
Akizngumza na wanajumuiya hayo profesa MBWETE amesema kuwa
CHUO Kikuu Huria nchini (OUT) kipo katika mchakato wa kufanya
maboresho ya mfumo wa utoaji wa elimu ambapo sasa kitaanzisha vyuo katika ngazi
ya mkoa (College).
Katika mabadiliko hayo
chuo hicho pia kitafungua matawi katika ngazi ya wilaya kwa kushirikiana na
Halmashauri za wilaya.
Amesema mchakato wa mabadiliko hayo tayari umepata Baraka
za Tume ya Vyuo Vikuu nchini na kwamba muda si mrefu OUT itaanzisha college
katika ngazi ya mikoa.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa OUT mkoa wa Temeke Dk. Jacquiline Bundala amesema tangu
kuanzishwa kwa kituo hicho mwaka 2007 chuo hicho kimepata mafanikio makubwa.
Ameyataja baadhi ya
mafanikio hayo ni pamoja na kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka wanafunzi 258
waliokuwepo wakati huo hadi zaidi ya 600 waliopo sasa.
Pamoja na mafanikio
hayo Dk. Bundala pia amesema chuo hicho mkoa wa Temeke kinakabiliwa na tatizo
la mtandao ambao ni nyenzo muhimu kwa ajili ya kujifunza.
Kata keki tule |
Kwa upande wake Rais wa Serikali ya wanafunzi
wa Chuo Kikuu Huria mkoa wa Temeke Malimi Ntegwa ameutaka uongozi wa chuo hicho
kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi ikiwemo tatizo la upatikanaji wa
vitambulisho, sehemu za kujifunzia hasa wakati wa vipindi vya ana kwa ana.
PICHA NYINGINE ZA HAFLA HIYO ZIPO CHINI
No comments:
Post a Comment