LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA WIKIENDI HII
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea wikiendi hii katika viwanja sita tofauti nchini, viwanja vinne vikitimua vumbi kesho jumamosi, na michezo miwili kuchezwa siku ya jumapili.
Jumamosi JKT Ruvu watakua wenyeji wa Coastal Union katika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es salaam, huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakiwakaribisha maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Timu ya Mtibwa Sugar watawakaribisha Azam FC kwenye uwanja wa Manungu-Turiani mjini Morogoro,nayo Ndanda FC watakua wenyeji wa timu ya Tanzania Prisons mjini Mtwara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Ligi hiyo itaendelea siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Young Africans watawakaribisha timu ya Mbeya City kutoka mkoani Mbeya, huku mjini Shinyanga katika uwanja wa Kambarage wenyeji timu ya Stand United wakiwakaribisha maafande wa timu ya Polisi Morogoro.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment