Sunday, April 5, 2015

DIWANI WA CCM HUKO KIJICHI AWAKUNA VIJANA,ADHAMINI LIGI YENYE DHAMANI YA MILLION 35

Diwani wa kata ya mtoni kijichi CCM mh ANDERSON CHALE kulia akimkabidhi jezi mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM katika kata hiyo bwana ABDALAH LIMBANGA ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa ligi ya mpira wa miguu katika kata hiyo ligi itakayojulikana kama UVCCM KIJICHI CUP ambayo yanatarajiwa kuanza takribani wiki mbili zijazo,picha ya chini inaonyesha akimkabidhi mipira ambayo imetolewa kwa kila timu kwa ajili ya kufanya maandalizi ya ligi hiyo

  Diwani wa kata ya mtoni kijichi mh ANDERSON CHALE leo amekabidhi vifaa vya michezo mbalimbali kwa timu 50 katika kata hiyo kama maandalizi ya ligi itakayoendeshwa katika kata hiyo na kujulikana kama UVCCM KIJICHI CUP.
Vifaa ambavyo vimekjabidhiwa kwa timu hizo ni jezi,ambapo kila tiku moja imepoatiwa jezi pamoja na mpira mmoja ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuanza baada ya wiki mbili na kuendeshwa na kata ya mtoni kijichi kwa kudhaminiwa na diwani huyo.
Mh diwani ANDERSON CHALE akionyesha pikipiki ambazo ni moja katika zawadi za washindi wa ligi hiyo,ambapo picha za chini zinaonyesha akimkabidhi pikipiki hizo mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM kwa ajili kabisha ya kushindaniwa katika ligi hiyo.
 Akizungumza na washiriki wa mashindano hayo ya mpira wa mguu mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM katika kata hiyo ndugu ABDALAH LIMBANGA amesema kuwa mashindano hayo yatashirikisha jumla ya timu hamsini ambapo kila mtaa katika kata hiyo umetoa timu kumi kwa ajili ya kushiriki katika mashindano hayo.
Amesema kuwa katika ligi hiyo ambayo inakadiriwa kutumia jumla  ya million 35 hadi kukamilika kwake washindi watapewa zawadi mbalimbali ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na pikipiki,jezi pea mbili pamoja na kombe ambapo mshindi wa pili na watatu watapata zawadi kemkem ikiwemo pikipiki moja kwa kila timu.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo diwani huyo amesema kuwa amesukumwa kudhamini mashindano hayo baada ya kugundua kuwa katika kata yake kuna vijana wengi na wanahitaji umoja ili waweze kujiletea maendeo na njia aliyoona ya kuwaunganisha kwa pamoja ni pamoja na kuanzisha mashindano kama hayo kwa lengo la kuwakutanisha vijana hao.


No comments: