Wanafunzi kutoka Shirikisho la elimu ya vyuo vikuu ambao ni makada wa chama cha Mapinduzi(CCM) mwishoni mwa juma hili wamejitokeza kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Kawe jijini Dar es salaam.
Akizungumzia operesheni hiyo Mwenyekiti wa shirikisho la elimu ya vyuo vikuu Iman Matabula amesema kuwa wamefanikiwa kupanda miti takribani 500, kufanya usafi katika zahanati ya Kawe pamoja na shuke ya msingi ya tumaini ambayo kuhistoria nidio shule ya mwisho ya mama salma kikwete kufundisha kabla ya kuwa first lady wa tanzania,na kufanya usafi katika maeneo ya masoko yaliyopo kawe pamoja na kuzungumza na wananchi.
Kwa upande wa mambo waliyozungumza na wananchi ni kuhimiza wajitokeze katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura pamoja kuwahimiza kuhakikisha kuwa wanalirejesha jimbo la Kawe lililokuwepo mikononi mwa Chama cha Demkrasia na Maendeleo Chadema.
Vijana hao pia walitoa misaada mbalimbali ikiwemo sabuni na vitu kama hivyo katika zahanati ya kawe na katika shule ya msingi tumaini waliahidi kuchangia tofali 500 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi katika shule hiyo..
TIZAMA PICHA ZA TUKIO NZIMA HAPO CHINI
Walipofika zahanati ya kawe |
No comments:
Post a Comment