Tuesday, April 21, 2015

DRFA YATANGAZA ZAWADI KWA WASHINDI WA LIGI YA WANAWAKE



Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimetangaza zawadi kwa washindi wa michuano ya ligi ya wanawake mkoa wa Dar es salaam inayoendelea katika viwanja mbalimbali Jijini.

Mwenyekiti wa chama hicho Almas Kasongo,amesema zawadi hizo zitatolewa kwa mshindi wa kwanza na wapili,mchezaji bora wa mashindano,mfungaji bora,kipa bora,timu yenye nidhamu na mwamuzi bora.

Mshindi wa kwanza atazawadiwa Kikombe,jezi seti moja  na kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000/=),Mshindi wa pili atapata jezi seti moja na kiasi cha shilingi laki saba (700,000/=) ,Mchezaji bora wa mashindano atazawadiwa kiasi cha shilingi laki mbili (200,000/=),Mfungaji bora atapata shilingi laki moja na nusu (150,000/=),Kipa bora atapata shilingi laki moja na nusu (150,000/=),Timu yenye nidhamu itazawadiwa shilingi laki nne (400,000/=),huku mwamuzi bora akiondoka na shilingi laki mbili (200,000/=).

Ligi hiyo yenye jumla ya timu 8 imeanza kutimua vumbi jumapili ya April 19/2015,kwa mchezo wa ufunguzi uliozikuwanisha timu za Temeke Squad dhidi ya Ever-Green Queens,na kushuhudiwa Ever-Green ikichomoza na ushindi wa kishindo wa mabao 5-1,yaliyofungwa na Sherida Boniface dakika ya 7,19na 39,na mengine yakifungwa na Donicia Daniel katika dakika ya 60 na 65,na lile la kufutia machozi kwa Temeke Squad likifungwa na Aisha Juma.
Tumi zote zinzoshiriki michuano hiyo ya ligi ya wanawako mkoa wa Dar es salaam ni pamoja na  
 
IMETOLEWA NA DRFA,
Omary Katanga Mkuu Wa Habari Na Mawasiliano,DRFA

No comments: