YANGA, ETOILE ZAINGIZA MIL 223
Mchezo no.91 wa Kombe la Shirkisho barani Afrika (CC) hatua ya 16 bora uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam, kati ya wenyeji timu ya Young Africans dhidi ya Etoile du Sahel kutoka Tunisia umeingiza jumla ya sh. 223,135,000.
Jumla ya watazamaji 36,105 walikata tiketi kuhudhuria mchezo huo, huku VIP A zikikatwa tiketi 68, VIP B tiketi 869, VIP C tiketi 582, Orange tiketi 1,955 na viti vya rangi ya Bluu na Kijani tiketi 32,631 ziliuzwa.
Mgawanyo wa mapato ni VAT 18% sh. 34,037,542.37, Gharama ya tiketi sh. 11,462,000, Gharama ya Uwanja 15% sh. 26,645,318.64, Gharama za mchezo 15% sh. 26.645,318.64, CAF 5% sh. 8,881,772.88, TFF 5% sh. 8,881,772.88 na Young Africans 60% sh. 106,581,274.58.
RUFAA YA NDUMBARO MEI 10
Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF iliyokutana Aprili 19, 2015 imepanga kusikilizwa kwa rufaa ya Damas Ndumbaro Mei 10 mwaka huu, makubaliano ambayo yalifikiwa na pande zote mbili kwa pamoja.
Kikao hicho kilipitisha taratibu za kisheria ambazo zitatumika kuamua kesi hiyo, ambazo ni taratibu kama zinazotumika mahakamani ikiwemo kuwasilisha hoja kwa mdomo na si maandishi, kitendo ambacho kimekubaliwa na pande zote mbili.
Utaratibu huu umekua ukitumika katika mahakama za kawaida kuepusha manung'uniko kwa upande mmoja kulalamika umeonewa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment