Uongozi wa kampuni ya
reli nchini Tanzania TRL leo umetangaza kuanza kwa safari ya pili ya treni yake
mpya (DELUX) iliyozinduliwa mnamo wiki
moja iliyopita ambapo safari hii ya pili itakuwa ni zamu ya kanda ya ziwa
ambapo itaelekea mwanza leo tarehe 12,mwezi wa nne.
Akizungumza na
wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam afisa uhusiano wa kampuni hiyo bwana
MIDIADJY MAEZ amesema kuwa safari hii ni ya pili kwa vile uzinduzi
ulishafanyika tarehe moja mwezi wa nne mwaka huu na kuelekea kigoma ziwa Tanganganyika
ambapo treni hiyo ilipokelewa kwa furaha mjini kigoma na sasa ni zamu ya mkoa
wa mwanza ambapo treni hiyo inafanya safari zake kwa wiki mara moja.
Afisa uhusiano wa kampuni hiyo bwana MIDIADJY MAEZ akizngumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam |
Amesema kuwa Treni hiyo
mpya ya kisasa itakuwa ikifanya safari zake kwa wiki mara moja ambapo itakuwa
ikiondoka Dar es salaam siku za jumapili kanzia saa mbili usiku ambapo itakuwa
ikipokezana kati ya miji ya kigoma na mwanza.
Aidha akizungumzia
habari ambazo zilisambazwa kuwa baada ya safari ya kwanza ya tren hiyo
kulishughudiwa uharibifu mkubwa ndani ya mabehewa hayo ya kisasa amesema kuwa
hakuna uharibifu mkubwa kama ilivyoripotiwa ila kilichotokea ni watu kutookuwa
na elimu ya kutosha ya kutumia baadhi ya vifa vilivyo ndani ya treni hiyo
ambapo amesema kwa sasa wamejipanga kwa kuwa na wahudumu wa kutosha ili
kuhakikisha kuwa usumbufu kama huo hautokei tena.
No comments:
Post a Comment