Huwenda leo umeskia
habari mbalimbali kwenye mitandao humu zikisema kuwa kiongozi mkuu wa chama
cha ACT wazalendo mh ZITTO KABWE amempeleka mwenyekiti wa chama cha democrasia
na maendeleo CHADEMA mh FREMAN MBOWE mahakamani
kisa ni kutumiana ujumbe mfupi wa simu wa vitisho.
Habari hizo zilikuwa
zinasema kuwa mwenyekiti wa CHADEMA alimtumia ujumbe mfupi wa maandishi mh
ZITTO KABWE ujumbe ambao ulikuwa unamtuhumu kuwa anatumika na chama cha
mapinduzi na serikali NA PIA ANAITUMIA act KAMA DARAJA TU ILA ANAENDA KUJIUNGA ccm na maneno ya kumtisha
mengi jambo ambali likamfanya MH ZITTO kwenda kutoa ripot mahakamani kwa
usalama wake ila habari hizo hazikutaja ni mahakama gani kesi hiyo imepelekwa.
Sasa ukweli uko hivi mtandao
huu uliposoma habari hizo kwenye baadhi ya blog ukaamua kumtafuta afisa habari
wa chama cha ACT ambaye ametuambia kuwa hakuna ukweli wowote wa habari hizo
ambapo amesema hata wao wanashangaa story hiyo inayoenea ina lengo gani zaidi
ya kuwagombanisha watu hao wawili.
Ndugu mwandishi hakuna
ukweli wowote kaka wa habari hizo hata sisi tunazisikia tu kwa juu juu hatujui
chanzo cha habari hizo,ila tunafwatilia kujua mtunzi wa habari hizo,ZITTO kama
mnavyojua yupo kwenye ziara ya kuimarisha chama chake mikoani na wala hajafika
mahakama yoyote sasa tunashangaa kwa
mambo hayo kuzushwa kiajabu ajabu.
Mitandao mingi ilidai
kuwa haya ni maelezo ya zitto ila hakuna ukweli wowote
"NIMEPOKEA UJUMBE WA SMS
KATIKA SIMU YANGU UJUMBE AMBAO SIO MZURI KIUKWELI NA UJUMBE UNAONESHA KUA
UMETOKA KWA MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE NAAMINI UJUMBE UMETOKA KWAKE
KWAKUA NAMBA YAKE YA SIMU NINAYO NA NILI SAVE KATIKA SIMU YANGU YA MAWASILIANO
KWA JINA LA MKT. MBOWE KWA MAANA YA MWENYEKITI MBOWE HIVYO NILIVYOPATA UJUMBE
JINA LILITOKEA HILO LA MTUMAJI NA KUJUA UJUMBE UMETOKA KWAKE NA NILIPO ANGALIA
CENTER NUMBER IMETUMIKA YA VODACOM NIKAJARIBU KUMPIGIA HAKUA AKIPOKEA SIMU
ZANGU LENGO LA KUMPIGIA NI KUTAKA KUPATA USHAHIDI NA UHAKIKA ZAIDI WA SAUTI
YAKE LAKINI HAKUA AKIPOKEA SIMU ZANGU NDIPO LEO ASUBUHI NIKAWASILISHA HII KESI
KATIKA VYOMBO VYA SHERIA ILI KUWEKA USALAMA JUU YA JAMBO HILI NIMEUMIA SANA
KUAMBIWA MIMI NI KIBARAKA WA CCM PIA NIMEAMBIWA KUA NIMEJIUNGA ACT WAZALENDO
KAMA DARAJA TU KUWAHADAA WANANCHI ILI NIHAMIE CCM
No comments:
Post a Comment