Wednesday, April 29, 2015

LHRC-SERIKALI IACHE MARA MOJA KUIPIGIA KAMPENI KATIBA PENDEKEZWA

Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho  Bi HELLEN KIJO BISIMBA Akizngumza na wanahabri leo jijini  Dar es salaam kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu mchakato wa kura y7a maoni juu ya katiba pendekezwa
 Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC kimesema kuwa kitendo cha serikali kuanza kupiga kampeni na kuwashawishi wananchi kuipigia katiba pendekezwa kura ua ndio ni ukiukwaji  mkubwa wa sheria na na kitendo ambacho kina lengo la kiuvuruga mchakato mzima kwani serikali haina mamlaka ya kufanya hivyo kisheria.
Mratibu wa katiba kutoka kituo hicho Bi ANNA HENGA akizngumzia mambo kadhaa ambayo wamekutana nayo walipokuwa nawazunguka katika mikoa mbalimbali kutoa elimu juu ya katiba pendekezwa
Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es  salaam Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho  Bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa kituo hicho  kimekuwa kikifwatilia kwa ukaribu kauli mbalimbali za viongozi wa serikali kuanzia kwa Mh Rais KIKWETE pamoja na mawaziri mbalimbali ambapo wamekuwa wakiendelea kupiga kampeni ya kuwahimiza wananchi kupiga kura ya ndio katika katiba inayopendekezwa.

Wanahabari waikichukua taarifa hiyo
Amesema kuwa uvunjaji huo wa sheria umejionyesha wazi katika sherehe za muungano zilizofanyika tarehe 26,mwezi wa nne jijini Dar es salaam ambapo kauli mbiu yake ilikuwa “MIAKA 51 YA MUUNGANO;TUDUMISHE AMANI NA MSHIKAMANO;PIGA KURA YA NDIO KATIBA PENDEKEZWA;SHIRIKI KATIKA UCHAGUZI MKUU”.huku mkurugenzi huyo akihoji kama ni sahihi kwa serikali kutumia vibaya madaraka na fursa za kitaifa kuvunja sheria kwa kuipigia kampeni katiba inayopendekezwa ilihali ikijua ni kinyume cha shheria.

Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria kuna makundi ambayo yanaruhusiwa kutoa elimu ya katiba pamoja na upigaji kura ambayo ni asasi za kiraia,taasisi au vikundi vya watu ambapo amesema kuwa serikali kujiingiza katika kampeni hizo tena kwa kutumia rasilimali za watu ni uvunjifu wa sheria wa moja kwa moja na unapaswa kukemewa kwa haraka.
Aidha amesema kuwa kuiacha serikali kuendelea kupiga kampeni ya kuwataka wananchi waipigie ndio katiba pendekezwa ni kuwaaminisha wananchi wafikiri kuwa kufanya kampeni ya kura ya hapana ni kosa kwa kuwa wananchi wengi wana imani na matamko ya serikali kuliko ya taasisi nyingine.
Aidha katika hatua nyingine mratibu wa katiba kutoka kituo hicho Bi ANNA HENGA amesema kuwa kituo  kimetoka kuzunguka nchi nzima kutoa elimu juu ya katiba ambapo amesema kuwa changamoto kubwa waliyokutana nayo ni pamoja na wananchi kuwa tayari wameshaaminishwa kupiga kura ya ndiyo  kampeni ambayo amesema kuwa inaratibiwa na wakuu wa mikoa na wa wilaya.
Kituo cha sheria kimeitaka serikali kuacha mara moja mchezo huo kwani ni kinyume cha sheria kwani unaweza kusababisha madhara baadae ambapo wamesema kuwa kazi ya serikali sasa ihakikishe kuwa  inasambaza kwa wingi nakala za katiba pendekezwa kwa wananchi iliwazidi kuisoma kwa makini ili waweze kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi yao.





No comments: