Mwenyekiti wa jumuiya hiyo SHEKH MUSSA KUNDECHA akizngumza wakati wa akitoa tamko hilo leo jijini Dar es salaam |
Wakati matukio
mbalimbali ya kukamatwa kwa viongozi na waislam nchini kwa sababu za
kujihusisha na ugaidi yakizidi kutokea Jumuiya ya taasisi za kiislam nchini Tanzania
wameibuka na kulaani vitendo hivyo vinavyofanywa na serikali kupitia jeshi la
polisi huku wakiitaka serikali kuwaomba
radhi waislaam kwa vitendo hivyo ambavyo wameviita ni vya uonevu na
udhalilishaji kwa waislam wote nchini.
Mapema leo akizungumza
na wanahabari mwenyekiti wa jumuiya hiyo SHEKH MUSSA KUNDECHA amesema kuwa
kumekuwa na matukio ya kamata kamata ambayo kwa viongozi wa kiislam,walimu wa
madrasa pamoja na watoto ambao wanasoma katika madrasa hizo vitendo ambavyo
amesema kuwa vinakiuka haki za binadamu,haki ya kikatiba,kisheria,na utu wa
mwislam huku amesema vitendo hivyo vinazidi kuchochea hasira kwa waialam hao na
kuhisi kwamba serikali ina mpango wa kuangamiza uislam nchini.
Amesema kuwa vitendo
hivyo vinavyoendelea katika mikoa mingi sasa nchini vinazidi kuwagawa
watanzania kwa misingi ya dini,na imani zao jambo ambalo amesema kuwa linaweza
kusababisha matatizo makubwa kama halitadhibitiwa huku awali.
Akitaja maeneo ambayo
kamata kamata hiyo imewathiri waislam wengi ni pamoja na mkoa wa Kilimanjaro ambapo
watoto na walimu wa madrasa wamekamatwa,mtwara,kilombero mkoani morogoro ambapo
watu waliingia msikitini saa tisa usiku na baada ya muda mchache polisi
wakaingia na kuwakamata jambo ambalo amesema bado linawapa shaka kuwa ulikuwa
ni mpango uliosukwa.
Naibu katibu mkuu wa Jumuiya na taasisi ya kiislam Tanzania, Rajab Katimba (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo |
Amesema kuwa hoja
inayoenezwa na serilakali kuwa wanazivamia madrasa kwa kuwa zipo kwenye hali duni
na hazina usajili haina maana kwa kuwa
hakuna sheria inayoonyesha jinsi na
vigezo vya kuzisajili huku akisema uduni wa madrasa hizo sio hoja kwani zipo
shule hadi wanafunzi wanakalia mawe lakini zimekuwa hazifungi wala kuvamiwa na
polisi.
Aidha amesema kuwa
kumekuwa na ugumu wa viongozi wao pindi wanapokamatwa na polisi kwa makosa kama
hayo ambayo ameita ya kusingiziwa ambapo swala la kuwapatia dhamana limekuwa ni
gumu sana na kinachofanyika ni kuwahamisha kutoka kituo kimoja kwenda kingine
huku wakiendelea kupatiwa mateso bila makosa ya msingi kutajwa.
Katika hatua nyingine
jumuiya hiyo imemtaka mkuu wa polisi nchini IGP,DPP,na kila kiongozi
anayehusika na utekelezaji wa matendo hayo kuchukua hatua za kujirekebisha na
kuacha kutekeleza uonevu huo dhidi ya waislaam.
Aidha amesema kuwa wao
kama waislaam wanaotetea waumini wao wamedhamiria kama ifikapo tarehe 15 mwezi ujao bila majibu sahihi ya
tamkio lao wamedhamiria kufanya maandamano ya amani kuishinikiza serikali
kuacha mara moja mpango huo ambao hauna tija kwa waislaam wala taifa kwa
ujumla.
No comments:
Post a Comment