Kama ulidhani matukio
ya kuchoma watu moto pale wanapokamatwa na makosa hususani ya kiijambazi ni kwa
baadhi ya maeneo unakosea sana,tukio hili limetokea leo mkoani kiilimanjaro
katika jimbo la vunjo maeneo ya mwika sokoni ambapo majambazi wawili ambao walikua
na silaha na kujaribu kupora lakini wananchi wenye hasira kali wakawashtukia na
kuwatia mikononi na kilichofwata ni mauaji ya kutisha.
Mashughuda wa tukio
hilo kutoka mwika sokoni ambao wamezungumza na mtandao huu wamedai kuwa majira
ya asubuhi kiukaribia mchana majambazo wannne walivamia eneo la maduka sokoni hapo karibu na
stendi ya magari ya kwenda moshi na kufwetua risasi hewani hovyo hovyo bila
mafanikio ndipo wananchi walifanikiwa kuwadhibiti majambazi lakini wawili
walifanikiwa kuchomoka na kutoweka na ndipo jumba bovu lilipowaangukia vijana
wawili na kukutana na unyama wa aiana yake.
Mashughuda wa tukio
wanazidi kutuambia kuwa baada ya kusalia wawili wananchi waliamua kufanya ukatili
wa aina yake baada ya kuamua kuwashushia kipigo cha mbwa mwizi na baadae kufanya
unayama mkubwa wa kumwagia mafuta ya taa na kumvisha tairi na kisha kumchoma
moto hali iliyoonyesha hasira za wananchi hao juu ya matukio ya ujambazi kama
hayo maeneo hayo.
Habari zinasema hadi
polisi wanafanikiwa kufika katika eneo la tukio kujaribu kuwatawanya wananchi
hao na kumuokoa kijana huyo walikuta tayari ameshakuwa kama mkaa jambo ambali
liliwafanya polisi kushindwa kufanya jambo zaidi ya kuchukua mwili wa kijana
huo na kuondoka nao.
SAMAHANI PICHA ZA CHINI KAMA HUTAMANI KUZIONA USIENDELEE
Mtandao huu bado
unafwatilia kwa ukaribu muendelezo wa tukio hili
No comments:
Post a Comment