Kampuni ya simu za
mkononi ya TIGO TANZANIA leo imezindua technologia mpya ijulikanayo kama 4G LTE
ambao utaifanya kuwa mtandao wa internent mkubwa na wenye kasi zaidi nchini.
Akizungumza katika
uzinduzi huo kaimu meneja mkuu wa TIGO CECILE
TIANO amesema kuwa kwa mara ya kwanza tena inaonyesha dhamira ya TIGO katika
kuleta mabadiliko ya maisha ya kidigitali na kama vinara katika matumizi ya tecnologia ya kisasa na ubunifu.
Kaimu meneja mkuu wa TIGO CECILE TIANO akizngumza katika nhafla hiyo |
Mtandao wa 4G LTE una
kasi ya haraka katika kupiga simu yani SKYPE kuperuzi na kupakua vitu mbalimbali
kutoka kwenye internent.Pia mtandao huo unaleta kitu kipya chenye huduma iliyo
bora zaidi kwa urushwaji wa video au kufanya mikutano kwa njia ya
mtandao.technologia hii mpya ina kasi ambayo ni mara tano zaidi ya technologia
iliyopo sasa kwenye soko ijulikanayo kama 3G.
Mkurugenzi mkuu wa TCRA Profesa JOHN NKOMA akizungumza kwa niaba ya malaka hiyo ambapo ameipongeza kampuni ya TIGO kwa huduma bora hususani hiyo waliyoizindua leo |
Kufwatia ongezeko kubwa
la matumizi ya simu za kisasa nchini zijulikanayo kama smartphones technologia
ya 4G itawezesha wateja wa TIGO kufurahia uzoefu huu wa kimataifa wa ongezeko
la kasi na ubora wa upatikanaji wa internent kwa njia ya mtandao
Waziri akiwasili katika ukumbi huo leo |
Amesema kuwa uzindiuzi
wa leo umejumuisha maeneo ya mliman city na masaki lakini lakini mpango wa tigo
ni kufikia maeneo yote ya Jiji la Dar es salaam ifikapo mwezi June kuhakikisha
kuwa upatikanaji wa huduma hiyo katika
wilaya za kinondoni,ilala na temeke hususani maeneo ya
Upanga,Tegeta,Mbagala,Tabata,Kimara,Mbezi,Ukonga,Salasala,Mikocheni,Msasani,Sinza,na
kadhalika.
Wasanii wa maigizo tanzania KITALE na STANBAKORA walikuwepo kufwatilia shughuli hiyo maalum |
Aidha ameongeza kuwa
watazindua huduma hiyo katika Miji ya Arusha,Moshi,Dodoma,Morogoro,Mwanza,na Tanga
ifikapo mwishoni mwa mwezi wa agosti.ambapo amesema hii itaifanya kampuni ya
tigo kuwa mtandao mkubwa wa 4G nchini Tanzania.
Akizindua huduma hiyo
ambayo ni mpya nchini waziri wa mawasiliano sayansi na technologia mh MAKAME
MBARAWA amesema kuwa ni hatua kubwa sana imefanywa na kampuni ya TIGO kwa
kuzindua huduma hiyo na inafaa kuigwa na makampuni mengine ili kuhakikisha kuwa
Tanzania nzima inakuwa na huduma hiyo ambayo itawasaidia watanzania kwa namna
moja ama nyingine.
VANESA MDEE msanii wa bongo flaver alikuwepo |
Amesema kuwa nchi kama Tanzania
kuwa na mtandao wenye uhakika na wa kasi ni fursa nzuri kwa vijana wake
kujiajiri katika shughuli mbalimbali zinazohusiana na mitandao kwani inakuwa
wamerahisishiwa kazi na kwa kuwa wana mtandao wenye kasi kama waliozindua
kampuni ya TIGO ni raisi zaidi kufanya hivyo
RICH MAVOKO msanii maarufu wa bongo fleva alikuwepo na akapata nafasi ya kutoa burudani kidogo |
Ameongeza kuwa serikali
ipo pamoja na kampuni ya TIGO kwa kuhakikisha kuwa huduma hiyo inaena katika
maeneo mengi ya nchi hadi vijijini ili lengo la kuifanya Tanzania iwe kama
kijiji liweze kutimizwa kikamilifu ambapo litasaidia katika shighuli mbalimbali
za kimaendeleo.
VABBESA MDEE akifwatilia muonekano wa video yake mpya unavyoonekana iwapo utaitizama katika mtandao wa 4G . PICHA NYINGINE NYINGI KUTOKA KWENYE HAFLA HIYO ZIKO HAPA |
No comments:
Post a Comment