Baadhi ya vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo
(Chadema) kutoka wilaya za Nyamagana, Magu, Busega na Bunda wameanza
matembezi ya siku sita kuelekea katika kijiji cha Butiama kwenye kaburi
la hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa lengo la kuwahamasisha
watanzania kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la
wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani
unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Matembezi haya ya vijana wa
Chadema yameanzia eneo la igoma jijini Mwanza, mahali
ambako mwaka 1967, Mwalimu Julius Kambarage
nyerere aliishia baada
ya
kutembea kwa miguu kutoka mwitongo, Butiama mkoani Mara akiunga mkono
azimio la Arusha.
Kiongozi wa msafara huo George
Charles ambaye ni mwenyekiti wa baraza la vijana wa Chadema (Bavicha)
kata ya igoma anasema lengo la matembezi hayo ya
zaidi ya kilometa 260 pamoja na mambo mengine ni kupinga ufisadi, mauaji
ya watu wenye ulemavu wa ngozi – Albino, vikundi vya kihalifu
vilivyoibuka jijini Dar es Salaam maarufu kama panya road, ambapo
wamelitaka jeshi la polisi kutowazuia na safari yao kwa vile matembezi
hayo ni ya amani kwa ajili ya kumuenzi baba wa taifa.
Baadhi
ya vijana wanaoshiriki matembezi hayo wanasema wameamua kufanya hivyo
kwa dhamira njema ili kuwahamasisha watanzania kujitokeza kujiandikisha
na pia kupinga uporaji wa raslimali za taifa unaodaiwa kufanywa na
baadhi ya watu wachache waliokabidhiwa dhamana ya uongozi na kusababisha
ufa mkubwa kati ya wenye nacho na wasionacho huku wananchi walio wengi
wakiendelea kukabiliwa na umaskini.
|
No comments:
Post a Comment