Waziri kivuli wa elimu na mafunzo ya ufunzi mh SUZAN LYIMO akizungumza na wanahabari leo juu ya mambo mbalimbali yanayoikabili nchi kwa sasa hususani secta ya elimu nchini |
Waziri kivuli wa elimu
na mafunzo ya ufundi mh SUZAN LYIMO ameitaka serikali iwebajibe ikiwa ni pamoja
na kuhakikisha vyakula vya kutosha vinafika mashuleni badala ya kutaka kuwawajibisha walimu wakuu ambao wamezuia
wanafunzi wao kurudi mashuleni kwa sababu za upungufu wa chakula kwani kufanya
hivyo ni kuwaonea kwa sababu walikuwa hawana njia mbadala ya kutatua tatizo
hilo.
Akizugumza na wanahabari
leo makao makuu ya chama cha Democrasia na maendeleo chadema Mh SUZAN LYIMO
amewapongeza walimu wakuu ambao wamewazuia wanafunzi wao kurudi mashuleni baada
ya likizo ya pasaka kutokana na kutokuwa na chakula katika shule zao hatua
ambayo amesema ni ya kijasriri nay a kmupongezwa kwani wasingefanya hivyo
wanhewez kuwasababishia wanafunzi matizo mengine kama ya migomo baada ya kukosa
vyakula mashuleni.
Amesema kuwa yeye kama
kama waziri kivuli wa elimu na mafunzo ya ufundi amekuwa akifwatilia swala hilo
kwa umakini na amefika hadi wizara ya TAMISEMI kutaka kupata majibu kuhusu
jambo hilo lakini amesema majibu aliyoyapata hayaridhishi kulinganisha na
ukubwa wa tatizo husika.
Aidha amesema kuwa
amezungumza na walimua wakuu ambao wamezifunga shule zao kutokana na ukosefu wa
chakula ambapo amesema kuwa walimu hao wamekana kuzifunga shule na badala yake
walichofanya ni kuongeza muda wa likizo kwa wanafunzi wao ili kusubiri
uwezekano wa kupata chakula kwa ajili ya wanafunzi hao kinyume na madai ya
serikali kuwa kuna walimu wamezifunga shule kinyume na sheria.
Katika sakata hilo
ambalo linaendelea shule mbalimbali nchini zikiwemo
malangali,mpwapwa,chanwe,ihungo,na nyingine nyingi zimeendelea na likizo ya
pasaka ili kusubiri uwepo wa chakula katika shule hizo.
Katika hatua nyingine
waziri huyo kivuli amesikitishwa sana na mfumo mbovu wa kuwapata walimu katika
vyuo mbalimbali nchini kwa mwka huu ambapo tofauti na miaka mingine wanafunzi
wamekuwa wakienda mafunzo ya vitendo kwa wiki zaidi ya tano lakini mwaka huu
wanafunzi wa ualimu wamehudhuria mafunzo ya vitendo kwa wiki tatu tu kwa sababu
ambazo zimetajwa kuwa ni kutokuwa na fedha za kutosha kuwapeleka wanafunzi hao
kwa wiki nane mfulilizo.
Amesema kuwa kwa mfumo
huo ni lazima tanzania itazidi kuporomoka kwa elimu kwa kuwa ni bora kuwa na
majengo mabovu lakini serikali iwe na walimu wenye ujuzi wa kutosha
kuwafundisha wanafunzi wake kwani kinyume na hapo kutazidi kuwa na anguko kubwa
la elimu.
No comments:
Post a Comment