Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Magalula Saidi katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Coastal Union na viongozi wa mkoa,kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union,Steven Mguto |
NA MWANDISHI
WETU,TANGA.
VIONGOZI
wa Klabu ya Coastal Union wamewatakiwa kushikamana vilivyo
ili
kuweza kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika michezo yao
iliyosalia
katika Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania Bara.
Wito
huo ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Magalula Saidi wakati
alipokutana
na viongozi wa timu hiyo ofisini kwa lengo la kufahamiana
ambapo
Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto aliwaongozwa
viongozi
wengine kwenye kikao hicho.
Alisema
kuwa muda uliobakia kwenye mechi za Ligi kuu sio wa kuanza
kufikiria
ni kitu gani kimetokea bali ni kuweka mipango imara na
madhubuti
itakayowapa mafanikio ili waweze kujipanga msimu ujao kwa
ligi
nyengine.
Aidha
aliwataka viongozi hao kujiepusha na migogoro, mifarakano
iliyokuwa
na tija kwani hali hiyo ikiruhusiwa itashindwa kuwapa
maendeleo
na kukwamisha mipango yao waliojiwekea.
Kwa
upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto
alimuhaidi
mkuu wa mkoa huyo kuyafanyia kazi kwa asilimia kubwa
maelekezo
aliyoyatoa ili waweze kupata mafanikio..
Naye,
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Coastal Union, Akida Machai
alisema
changamoto zilizojitokeza kwenye michuano hiyo watazifanyia
kazi
kwa umakini mkubwa ili ziweze kuleta ufanisi katika michezo
iliyosalia.
Kikao
hicho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa soka akiwemo
Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho la soka Nchini (TFF) Khalid
Abdallah.
No comments:
Post a Comment