Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo,Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo, Mehul Asher akizungumza leo ofisini kwake,Picha na Mpiga Picha Wetu |
NA MWANDISHI WETU, TANGA.
MASHINDANO
ya mbio za Magari ya “Zig Zag Tanga Rally 2015”
yanatarajiwa
kuanza kutimua vumbi mkoani Tanga Mei 3 mwaka huu
mzunguko
wa pili kwenye yale ya Kitaifa chini ya ufadhili wa Zig Zag.
Mashindano
hayo watashindanisha umbali wa km 135 na yatakuwa na awamu
tano,
yatakayoanzia katika hotel ya Tanga Beach Resort na kupitia
maeneo
ya Pongwe, Mkanyageni na Mjesani na kurudi yalipoanzia.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya
Mashindano
hayo, Mehul Asher alisema kuwa maandalizi yanaendelea
vizuri
ambapo washiriki kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.
Alisema
kuwa madereva watakaoshiriki katika michuano hiyo wanatazamiwa
kutoka
mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga
ikiwemo
wengine kutoka nchi za Kenya na Uganda.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa mashindano hayo msimu huu yatakuwa na
upinzani
mkubwa kutokana na barabara watakazotumia washiriki ni nzuri
hivyo
itaweze kuwapa fursa kushindana vema.
Aidha
alisema kuwa makabidhiano ya zawadi zilizoandaliwa kwa washindi
mbalimbali
zitafanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly
mara
baada ya kumalizika mashindano hayo.
Hata
hivyo alisema kuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo anatarajiwa
kuwa
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Dr.Fennela
Mukangara
No comments:
Post a Comment