SERIKALI YA TANZANIA
ICHUKUE HATUA ZA HARAKA KUNUSURU WATANZANIA WAISHIO AFRIKA KUSINI DHIDI YA
GHASIA NCHINI HUMO
Kumekuwepo na hali ya
raia wa Afrika Kusini kushambulia , kujeruhi na kuua raia wa kigeni wa Kiafrika
wanaoishi nchini Afrika Kusini.
Hali hii inadaiwa
kuchochewa na ukosefu mkubwa wa ajira kwa wananchi wa Afrika Kusini wanaodai
ajira hizo kuchukuliwa na Waafrika wa mataifa mengine na hivyo wao wenyeji
kubakia kwenye dimbwi kuu la umasikini.
Ni mtazamo wa kuimarika
kwa kiwango cha umasikini kwa wananchi wengi nchini humo dhidi ya kuimarika kwa
kiwango cha utajiri kwa wachache kunakopelekea ghasia hizi
Zaidi, mali za Waafrika
wageni nchini humo zimekuwa zikiharibiwa
baada ya wamiliki kukoswa katika mashambulizi hayo.
Aidha, kama nchi
nyingine za Kiafrika, Tanzania ina idadi kubwa ya raia wake wanaoishi nakufanya
kazi nchini Afrika Kusini. Na mpaka sasa inadaiwa kuwa watanzania wawili (2)
wameuwawa katika ghasia hizo za wenyeji dhidi ya Waafrika wageni.
Kwa misingi hiyo:
1.
CHADEMA inalaani vikali hali ya raia
kudhuru na kutwaa uhai wa raia yoyote yule. CHADEMA kama muumini wa haki za
binadamu inayojumuisha haki kuu ya kuishi inasikitishwa na hali hiyo ya
machafuko inayoondoa usalama wa sio tu kwa raia wa kigeni wa Kiafrika walioko
Afrika Kusini bali pia kwa raia wengine wa Afrika Kusini ambao hawawezi kufanya
shughuli zao kwa ukosefu wa usalama nchini humo.
CHADEMA
inawasii raia wa Afrika Kusini kuwachukulia Waafrika wenzao kutoka mataifa
mengine kama ndugu zao ambao kwapamoja walishrikiana kupambana na ubaguzi wa
rangi na hatimaye kuleta uhuru kwa taifa
hilo. Ni muhimu raia wa Afrika Kusini wakatatua matatizo yao ya ndani hasa ya kiuchumi kwa kushirikina na wenzao wa
mataifa ya Afrika waishio nchini humo na si kuwaona kama maadui zao.
2.
CHADEMA inaitaka serikali ya Tanzania
ishirikiane na serikali ya Afrika Kusini kuchukua hatua za haraka kunusuru
maisha ya watanzania waishio nchini Afrika Kusini dhidi ya ghasia hizi kwa
kuwahakikishia usalama wao ama kuwawekea utaratibu wa kuondoka ama nchini humo
na kurejea nyumbani ama kwenye miji yenye machafuko kama Durban na kuwapeleka
kwenye miji ya usalama zaidi mpaka hali itakapotengamaa kwenye miji hiyo kama
ilivyofanya kwa Watanzania waishio Yemen ambako nako machafuko yamekithiri.
Ni
muhimu Serikali ikawa makini kwa jambo hili kwani teyari mataifa mengine ya
kiafrika ya Botswana, Malawi na Zimbabwe yaneshaanza kuwaondoa raia wake nchini
humo kwa kuhofia usalama wao.
3.
CHADEMA inazikumbusha nchi za Kiafrika
ambazo zina utajiri mkubwa wa rasilimali kuhakikisha inatatua matatizo ya
kiuchumi yanayozikabili nchi hizo ikiwa ni pamoja na kupunguza tofauti ya
kipato kati ya wengi wasio nacho na wachache wenye nacho.
Ni
muhimu serikali hizi kujikita katika kupambana na umasikini kwa kutengeneza
fursa za ajira kwa raia wake na hivyo kupunguza kiwango cha umasikini na
hatimaye kuondoa mazingira ya machafuko yanayosababishwa na hasira za wananchi
kutokana na hali yao ya umasikini.
Kwa
mantiki hiyo, ni muhimu Jumuiya za kikanda na Umoja wa Afrika wenyewe (AU)
zikaweka msisitizo wa ukombozi wa kiuchumi unawaweza kukidhi haja na matakwa ya
raia wa bara hili.
4.
Kipekee, CHADEMA inaikumbusha serikali
ya Tanzania kuichukilia hali ya Afrika Kusini kama taadhari kwake kwani hali ya umasikini na
ukosefu wa ajira hapa nchini imekuwa kubwa kiasi cha kuibuka kwa vikundi vya
kihalifu vya Komando Yoso na Panya Road vilivyofanya mashambulizi na uporaji
kwa raia wengine. Tofauti ndogo iliyopo kati ya Afrika Kusini na Tanzania ni
kwamba Afrika Kusini raia wazalendo wanashambulia waafrika wa mataifa mengine
wakati hapa Tanzania ilikuwa ni kushambuliana baina ya Watanzania.
Imetolewa leo tarehe 18.04.2015
Jijini Dar es salaam na;
Deogratias Munishi
Mkuu wa Mambo ya Nje –
CHADEMA
+255715887712
No comments:
Post a Comment