Friday, May 1, 2015

WAZIRI MWAKYEMBE AWAPONGEZA WACHEZA BAO NCHINI

Na Mwandishi wetu

WAZIRI wa Wizara ya Afrika mashariki,Harison Mwakyembe amelipongeza Shirikisho la Mchezo wa bao nchini (Shimbata) kufuatia kudumisha utamaduni wa ndani.
Hayo yalisemwa Dar es salaam jana,na Waziri huyo alipokuwa akikabidhi zawadi za washindi wa kombe hilo la mchezo wa bao ambapo  Abdalah Said wa Temeke aliibuka mshindi wa kwanza na kukabidhiwa kiasi cha sh 500,000,na Abdalah  Machupa akishika nafasi ya pili na kupata sh 300,000,na nafasi ya tatu ilichukua na Mlaponi amabye alipewa sh 200,000.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi zawadi za washindi wa kombe e  hilo la muungano ,pamoja na wajumbe wa chama hicho,Waziri Mwakyembe alisema kuwa mchezo wa bao ni mchezo pekee wa tamaduni  ya Tanzania hivyo serikali kuna haja ya kuwapa nguvu za kutosha,pia na wapongeza sana.


No comments: