Katika jitihada za kuijengea jamii ya kitanzania tabia ya
kufanya mazoezi kwa ajili ya kuboresha afya zao, kampuni ya Fern (T) Ltd
imeandaa tamasha la kimichezo litakaloambatana na mazoezi pamoja na burudani
kwa ajili ya watu wa kada mbali mbali.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo, mratibu wa tamasha hilo DIMO DEBWE MITIKI amesema Lengo
kubwa la tamasha hilo, ni kuwakutanisha pamoja watu wa kariba mbalimbali na
umri tofauti kufurahi pamaja na kuweka miili yao fit na kuongeza kuwa,
watakuwepo wataalamu mbalimbali waliobobea kwenye sekta ya ufundishaji juu ya
ufanyaji mazoezi na wataalamu wa afya watakaotoa ushauri mbalimbali wa afya na
lishe.
“Kwa siku za hivi karibuni watu
wengi wamekuwa wakifuatilia sana masuala ya afya kitu ambacho kimepelekea
kuibuka kwa vikundi vingi/vilabu vingi vya mazoezi. Kutokana na kutokuwepo kwa
muundo rasmi unaowakutanisha watu hawa wapenda mazoezi Fern imetambua na kuona
fursa hiyo kupitia Tamasha la jumapili la mazoezi litafanyika siku ya jumapili
ya tarehe 14 mwezi Juni,2015 katika viwanja vya LEADERS CLUB Kuanzia saa 12
asubuhi mpaka saa 12 za jioni,” alisema
Moja kati ta waratibu wa Tamasha hilo JOSEPHINE KAYOMBO akizungumza na wanahabari mapema leo juu ya maandalizi ya Tamasha hilo |
MITIKI ametaja washiriki wa
tamasha hilo kuwa ni pampja na Joging clubs zaidi ya 100 kutoka wilaya zote 3
za mkoa wa Dar es Salaam; Temeke,Kinondoni na Ilala, makampuni na Taasisi
mbalimbali wakiwemo, CRDB Bank, TCDC, SMART TELECOMMUNICATION, PSI n.k
Amesema washiriki wengine ni
pamoja na Gyms kama vile AZURA, THE GYM, GENESIS HEALTH CENTRE, POWER ON
FITNESS, HOME GYM NA UNIVERSAL GYM, wasanii wa tasnia ya Filamu na Muziki
nchini.
“Kutakuwa na shughuli mbali mbali
zitakazokuwa zikiendelea wakati wa tamasha .Baada ya watu wote kukusanyika
tutafanya jogging kwa pamoja tukianzia viwanja vya leaders kuelekea Coco beach
na kuzunguka maeneo ya kinondoni kisha kurudi tena Leaders na baada ya watu
kurudi leaders tutaendelea na mazoezi ya viungo (AEROBIC) kwa muda wa lisaa
limoja.
Zoezi hili likimalizika litafuatiwa na kipindi cha dondoo
za lishe na afya kutoka kwa kwa wataalamu waliobobea ambapo watu watapata fursa
wa kujifunza mambo kadhaa yahusuyo afya,” alifafanua
Ameongeza kuwa, uduma za chakula
na vinywaji zitapatikana huku burudani kutoka kwa wakongwe wa muziki wa dansi
nchini Bendi ya TWANGA PEPETA
watakuwepo kuisindikiza siku hii mahususi.
“Watu wa rika zote mnakaribishwa
kuja kushiriki kwenye Tamasha hili la kipekee hakuna kiingilio ni bure kabisa.
Njooni tuungane kwa pamoja kwa
kuweka miili yetu fit, kutengeneza fursa
kwa kujenga mahusiano na wadau mbalimbali,” aliongeza
Tamasha limedhaminiwa na CRDB
BANK, TIGO, COCA COLA pamoja na CLOUDS FM
No comments:
Post a Comment