Meneja Mkuu wa kampuni ya fastjet, Afrika masharaki, Jimmy kibati akizungumza katika semina hiyo |
Kampuni ya fastjet ambayo ni kampuni ya ndege ya kiafrika yenye gharama nafuu, imeingia kwenye mkakati kabambe wenye lengo la kuongeza idadi ya wateja kwa kuweka bei za chini kabisa katika safari za anga barani Afrika.
Sambamba na mkakati huu, Kampuni ya Fastjet itakuwa ikifanya kampeni za mara kwa mara kwa wateja kwa lengo la kuwaelimisha wasafiri wa anga namna bora za kupata bei za tiketi halisi.
Tulifanya tafiti nyingi za wateja juu ya changamoto wanazokutana nazo wasafiri wakati wakifanya taratibu za kukata tiketi kwa ajili ya safari za ndege, mojawapo kubwa kabisa ilikuwa ni ongezeko la bei za tiketi kwa mawakala watapeli. Kwa mantiki hii tunataka kujenga uelewa juu ya jinsi watumiaji wanaweza kupata kilicho bora kwa fedha zinazotumika, "alisema Meneja Mkuu wa Fastjet, Afrika Mashariki, Jimmy Kibati.
Afisa Mahusiano na Masoko wa Kampuni ya ndege ya Fastjet, Lucy Mbogoro akielezea zaidi kuhusu kampeni ya Dili Bomba katika semina hiyo.
|
Usafiri wa anga wenye gharama nafuu ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi barani Afrika hasa katika sekta ya biashara na utalii, anasema Jimmy Kibati, Meneja Mkuu wa Fastjet kwa Afrika Mashariki, ambaye pia aliona, "Tunataka wasafiri kupata bei sahihi za tiketi. Tunataka iwe aina ya sekta ambayo kila msafiri atapata bei halisi.
Tayari kuna nauli kubwa mno zinazotozwa na makampuni ya ndege kwenye njia nyingi ikiwa ni pamoja na bei kubwa inayotolewa na wanaojifanya mawakala wa usafiri, ambayo inasababisha idadi ya raia wengi nchini kutokufurahia safari za anga na kuona faida zake katika kuokoa muda. aliongeza Kibati.
Kwa mujibu wa Kibati, fastjet imepiga hatua kubwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2015. Katika mwezi wa Aprili 2015, ndege ilisafirisha abiria wapatao 68,088, hii ikiwa ni idadi kubwa ya abiria kusafiri kwa mwezi tangu kuanza kwa shughuli za fastjet ikiwa ni pamoja na asilimia 92 ya utendaji mzuri kwenye suala la kujali muda kwa mwezi huo huo, ikijijengea yenyewe kuwa ni ndege ya uhakika na yenye bei nafuu.
Sambamba na usafiri wa anga kwa bei nafuu barani Afrika, Kibati alielezea, "Tunaamini kwamba kuna haja kubwa kwetu sisi kuwa aina ya ndege yenye gharama nafuu barani Afrika. Nia yetu ni kufanya kazi na serikali katika bara zima ili kuleta faida ya ushindani katika sekta ya anga. Hii itasababisha kuleta unafuu wa nauli kwa abiria. "
Kampuni ya fastjet ilianza shughuri zake za kibiashara tarehe 29 Novemba 2012, ikisafirisha abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro na Mwanza nchini Tanzania kwa ndege yake A319. Tangu wakati huo, ndege imepanua wigo wa mtandao wake na kuwa na njia tano ndani ya Tanzania. Kimataifa ndege ya Fastjet kwa sasa inasafirisha abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini, Lusaka nchini Zambia, Harare nchini Zimbabwe na Entebbe nchini Uganda.
Nauli za Fastjet kwa safari za ndani nchini Tanzania zinaanzia dola za kimarekani 20 kwa kwenda tu, na nauli kwa safari za kimataifa zinagharimu kuanzia dola za kimarekani 50 kwa mara moja tu, zote kwa pamoja ukiondoa kodi za uwanja wa ndege na serikali.
Mshauri wa Kibiashara wa Fastjet, Ian Petrie akielezea zaidi kuhusu kampeni ya Dili Bomba katika semina hiyo.
|
Pamoja na unafuu wa gharama zake za nauli, Kampuni ya fastjet inaamini inafanya usafiri wa anga kupatikana kwa Waafrika wengi zaidi. Ili Kusaidia imani hii, ni utafiti uliofanywa na kampuni muda mfupi baada ya uzinduzi wake, ambapo ilionyesha kuwa asilimia 38 ya abiria wake walikuwa ni mara yao ya kwanza kusafiri na ndege, ambao kabla hawakuwa hata na uwezo wa kumudu kusafiri kwa ndege.
Utaratibu wa ukataji wa tiketi katika kampuni ya Fastjet kutoka Tanzania unaweza kufanyika kimtandao kupitiawww.fastjet.com/tz ambapo nauli ya bei nafuu hutolewa, pia kupitia ofisi yoyote ya fastjet au kupitia mawakala wa usafiri. Malipo ya tiketi yanaweza kufanyika kwa pesa taslimu, kimtandao kwa kutumia kadi ya mkopo au kupitia Mpesa na TigoPesa.
No comments:
Post a Comment