Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Uchukuzi wa Egypt, Hossam Kamal, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sharm El Sheikh, jijini Sharm El Sheikh Cairo Misri, kwa ajili ya kuhudhuri Mkutano Mkuu wa tatu wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Soko la pamoja la nchi za Kusini mwa Afrika (COMESA) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Agenda ya mkutano huo ni kupokea taarifa ya majadiliano ya kuanzisha eneo huru la Biashara la Utatu wa EAC, COMESA na SADC. Picha na OMR
|
No comments:
Post a Comment