Tuesday, June 9, 2015

TAARIFA YA KUAHIRISHWA TRENI YA KUTOKA DAR ES SALAAM LEO

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika kuwataarifu wananchi na abiria waliokuwa wasafiri na treni ya leo Juni 09, 2015 kutoka Dar es Salaam kwenda bara kuwa safari hiyo imeahirishwa hadi kesho Jumatano saa 11 jioni.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kuahirishwa safari hiyo ni ajali ya treni ya mizigo iliyotokea usiku wa kuamkia leo Jumanne Juni 09, 2015 maeneo ya Stesheni za Ngeta na Ruvu mkoani Pwani ambapo mabehewa matano yenye shehena ya sukari yameanguka kabisa.

Tayari Wahandisi wa TRL wako eneo la ajali kufanya tathmini na kuanza zoezi la uokoaji, ikiwemo kazi ya kuyanyanyua mabehewa yaliyopata ajali na kisha kukarabati njia ili iwezwe kupitika mapema hapo kesho.

Uongozi wa TRL inawaomba radhi wananchi na wateja wake wote nchini kwa usumbufu utakaojitokeza.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya 

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ,

Mhandisi Elias Mshana,

Dar es Salaam,

Juni 09, 2015.

No comments: