MAFANIKIO
YA OPARESHENI YA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI JIJINI DAR ES SALAAM KAMA IFUATAVYO.
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na oparesheni kamambe ya
kuwasaka na kuwakamata majambazi wa kutumia silaha pamoja na uhalifu mwingine
ili kuhakikisha wananchi wa jiji la Dar es Salaam wanaishi na kufanya shughuli
zao za kila siku bila hofu ya uhalifu. Katika oparesheni hiyo, Jeshi limepata
mafanikio yafuatayo:
KUKAMATWA
SILAHA AINA YA AK.47 NA RISASI 13
Tarehe 09/06/2015 saa
08:45hrs asubuhi maeneo ya Yombo Relini (W) kipolisi Buguruni (M) wa Kipolisi
Ilala polisi kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kukamata silaha aina ya
AK47 yenye namba M73B1-130887 ikiwa na magazine yenye risasi 13.
Mafanikio haya
yalipatikana baada ya majambazi watatu kumvamia mtu mmoja DHARAMPAL S/O
NARALADE, Miaka 32, Mhasibu wa Kampuni ya Mohamed Enterprises mara alipotoka
getini katika ghala la kampuni hiyo lililopo Kiwalani Bombom na kisha kumpora
begi dogo ndani yake kulikuwa na kompyuta mpakato (laptop).
Baada ya uporaji
wananchi walitoa taarifa polisi. Polisi kwa kushirikiana na wananchi
waliyafuatilia majambazi hayo yaliyokuwa na pikipiki mbili zenye namba MC467 AKR Boxer nyekundu na MC274 ASS
Boxer nyeusi hadi maeneo ya Kiwalani relini ambako walitelekeza pikipiki
hizo. Wananchi wenye hasira kali waliweza kumshambulia jambazi aliyekuwa na silaha
kwa mawe na polisi waliweza kuwazuia lakini kwa bahati mbaya majeraha aliyokuwa
ameyapata yalisababisha kifo chake.
Majambazi wengine
walikimbia kabla hawajakamatwa. Pikipiki zinashikiliwa kituo cha Polisi
Buguruni kwa uchunguzi na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Temeke.
KUKAMATWA
KWA
BASTOLA NA RISASI ZAKE SITA
Katika hatua nyingine
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekamata bunduki nyingine aina
ya BASTOLA yenye namba za usajili TZCAR
91456 ikiwa na magazine yenye risasi sita ndani yake.
Tukio hili lilitokea
tarehe 08/06/2015 majira ya saa nane mchana maeneo ya Tabata Ubaya (W) kipolisi
Buguruni (M) Ilala Polisi waliweka mtego kwa lengo la kukamata kundi la vijana
baada ya kupokea taarifa kuwa kundi hilo linapanga kwenda kufanya tukio ka
uhalifu.
Baada ya askari kanzu
kuweka mtego ili kuwanasa vijana hao walistuka na kukikimbi ambapo walidondosha
silaha tajwa hapo juu. Uchunguzi
unaendelea ili kujua mmiliki halali wa silaha hiyo ikiwa ni pamoja na
kuwasaka watu hao.
KUKAMATWA
KWA POMBE YA MOSHI (GONGO) NA BHANGI JIJINI DAR ES SALAAM
Kumekuwa na ongezeko
la ukamataji wa wauzaji na watumiaji ya bhangi na pombe haramu ya moshi (gongo)
katika jiji la Dar es Salaam ambapo vinaathiri maisha ya vijana wengi.
Kwa mfano kwa tarehe
08/06/2015 peke yake walikamatwa watuhumiwa 161 kwa makosa ya kuvuta bangi, kunywa gongo na kuuza vitu hizi.
Aidha, kwa tarehe hiyo
hiyo zilikamatwa jumla ya lita 131 za
gongo, Puli 70 za bhangi, misokoto ya bhangi 205 na kete 395 za bhangi.
Nawashauri wauzaji, watumiaji,
na jamii kwa ujumla kutafuta shughuli nyingine mbadala za kujiingizia kipato
kuliko kufanya biashara ya kuuza gongo na bhangi ambazo ni kinyume cha sheria
za nchi. Nawashauri wazazi kutimiza wajibu wao wa malezi mazuri kwa vijana ili
kuwa na kizazi thabiti kwa maendeleo ya taifa la Tanzania.
S. N. SIRRO
NAIBU KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
NAIBU KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment