Chama cha wananchi CUF kimesema kuwa siku ya Jumapili ya Tarehe 14 mwezi huu wa sita ndiyo siku rasmi ya kumkabidhi rasmi form ya kuomba kugombea
urais wa jamhuri ya muunganoi wa Tanzania mwenyekiti wa chama hicho Profesa
IBRAHIM LIPUMBA baada ya kujitokeza mwenyewe katika chama hicho kuomba nafasi
hiyo licha ya chama hicho kutangaza kwa muda mrefu watu kujitokeza kutangaza
nia.
Amesema kuwa chama hicho
kulikuwa na utaratibu tofauti ambapo kilipanga kuwa baada ya wanachama wote
kuchukua form za urais kingewakutanisha kwa pamoja na kuwakabidhi form katika
mkutano mkubwa lakini kwa kuwa mwanachama aliyejitokeza ni mmoja haina budi
kufanya mkutano huo ambao utafanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa ubungio
plaza na kurushwa na television mbalimbali nchini Tanzania.
Katika hatua nyingine
mketo amesema kuwa katika nafasi za ubunge na madiwani hadi kufikia sasa chama
hicho kimekamilisha uchaguzi katika majimbo 133 kati ya 189 ambapo amesema kuwa
mchakato huo unaendelea kuwapata wagombea ambao watapelekwa katika meza ya
ukawa na kupatikana wale watakaogombea kupitia UKAWA.
Kwa maana hiyo profesa
IBRAHIMU LIPUMBA ndiye atakeyepambanishwa na wagombea wengine wa vyama vya
ukawa kumtafuta mgombea mmoja wa umoja huo katika nafasi ya urais
No comments:
Post a Comment