PICHA NA MAKTABA.
Story kubwa leo katika
Jiji la Dar es salaam hususani katika tasnia ya siasa ilikuwa ni mkutano mkubwa
uliofanyika katika ukumbi wa ubungo plaza wa chama cha wananchi CUF mkutano
uliokuwa na lengo la kumkabidhi form ya kuomba ridhaa ya kugombea urais wa
Tanzania kupitia chama hicho ambapo mgombea alikuwa ni mwenyekiti wa chama
hicho mwenyewe Profesa IBRAHIM HAROUNA LIPUMBA.
Hapa nimekuwekea baadhi
ya sentens ambazo mwenyekiti huyo alizizungumza katika hotuba yake ya kuomba
ridhaa ya wanachama wa chama hicho ili jina lake liweze kupelekwa katika meza
ya UKAWA.
1-Watu wanauliza
kwanini nangangania kuchukua form kwa mara ya tano tena,mwaka huu ni tofauti
sana na chaguzi ziingine,ni mwaka wa kufanya maamuzi ya ukweli juu ya nchi
yetu,nachukua form kipindi ambacho nchi ipo katika hali mbaya ya kiuchumi na
iko wazi kuwa sasa nchi imechoka.
2-Mimi ni mchumi ambaye
nimetumika sana na mataifa m
akubwa katika kuwashauri katika maswala ya kiuchumi
na wakafanikiwa kupitia kwangu,nadhani sasa ni wakati wa kujenga uchumi wa
Tanzania yangu mimi nikifanikiwa kuwa Rais ntahakikisha tunajenga uchumi
utakaomsaidia kila mtanzania.
3-Ntahakikisha kuwa
watoto wa Tanzania wanapata fursa ya kupata matunzo ya uhakika,ntasimamia
katika lishe ya watoto na mama wajawazito ili tujenge taifa imara,tofauti na
sasa ambapo watoto wa Tanzania muonekano wa vimo vyao haulingani hata kidogo na
umri wao,wengi wanakosa lishe bora wakiwa wadogo na hakina anayeliona hilo kwa
sasa.
4-Suala la ajira ni
tatizo kubwa sasa,nkifanikiwa kuiongoza Tanzania ntahakikisha kuwa tunatengeza
mazingira yatakayotoa fursa za ajira kwa vijana wa kitanzania kwa wingi.tutahakikisha
swala la miundombinu linarejkebishwa kwani ndio msingi wa kutengeneza
ajira,kama tukiwa na miundombinu bora najua maswala ya gesi na kilimo vitafika
kila eneo na ajira zitakuwepo kwa wingi.
5-Hali ya afya Tanzania
ni mbaya sana,bado kuna matatizo makubwa sana katika secta ya afya,Tanzania
inahitaji hifadhi ya jamii hususani kwa wazee wa Tanzania bado wanateseka sana
na swala la afya.
6-Maswala ya ufisadi
nchini Tanzania ni Tatizo sugu ambalo serikali ya ccm wameshindwa kulifanyia
kazi,hao wanaotuibia kila siku ndio hao wako mtaani wanatangaza nia,wangetakiwa
wote wawe jela wanatumikia kifungo.mimi nikichukua hii nchi sitacheka na
mafisadi kama hao nakamata wote naweka ndani.
7-Swala la katiba mpya
ntahakikisha tunauanza mchakato upya huku tukiyaheshimu maoni yaliyotolewa na
wananchi na sio matakwa ya watu flani.
8-Kama UKAWA
wakimchagua mtu mwingine kusimama katika nafasi ya urais naahidi kuwa ntakuwa
naye bega kwa bega kumpigania hadi tuikomboe Tanzania.
9-Mwisho namaliza kwa
kusema kuwa watanzania tuende tukajiandikishe kwa wingi katika daftari la
kudumu la wapiga kura ili mwaka huu uwe ni mwaka wa maamuzi kweli.
|
No comments:
Post a Comment