Mtoto ANTHONIA SANGEDA kutoka shule ya ST MARRY MAZINDE JUU akizungumza na wanahabari wakati wakisoma tamko lao juu ya siku ya mtoto wa Africa na changamoto zinazowakabili wao kama watoto |
Ikiwa leo ni siku ya
maadhimisho ya siku ya Mtoto katika bara la Africa serikali ya Tanzania imetakiwa
kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kuwa haki ya motto wa kitanzania
inatambulika na kuthaminiwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa watoto
wanatambulika katika katiba na sheria mbalimbali ili kuwasaidia kuypata haki
zao za msingi.
Wito huo umetolewa na
watoto mbalimbali waliopo katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa afica ambayo
wanayafanyia kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC wakati wakitoa tamko kwa
vyombo vya habari kuhusu siku ya mtoto wa Africa.
Wamesema kuwa wanaamini
ikiwa serikali itaamua kwa dhati kuweka mfumo mzuri ambao utamuwezesha mtoto kuwa
katika mazingira salama itakuwa ni hatua mbadala ya kumlinda mtoto wa
kitanzania ikiwa ni pamoja na kuwepo mfumo imara wa mawasiliano ambao utamwezesha mtoto kufikisha
maoni yake katika ngazi husika pale ambapo atakuwa anakosa haki zake za msingi.
Mtoto CHANDE MOHAMED kutoka shule ya PENDAMOYO Jijini DAR ES SALAAM akizngumza na wanahabari |
Katika tamko hilo limeanisha
mambo mbalimbali ambayo bado ni changamoto kwa watoto wa kitanzania huku kubwa
likiwa ni tatizo la mimba za utotoni ambalo kwa kipindi cha hivi karibuni
limeshika kasi sana na kuleta madhara makubwa kwa watoto wengi ikiwa ni pamoja
na kuwaharibia ndoto zao za kimaisha.
Wameeleza kuwa matatizo
hayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakisababishwa na kutokuwepo kwa mfumo inara wa
ulinzi kwa mtoto hasa kwa watoto wa kike,kutokuwepo kwa mfumo wa utoaji elimu
kwa jamii ya watanzania juu ya haki za mtoto,pamoja na kutokuhukumiwa kwa
watuhumiwa wanaokiuka sheria za haki ya mtoto.
Wanafunzi mbalimbali waliohudhuria kuadhimisha siku ya mtoto wa Africa makao makuu ya kituo cha sheria na haki za Binadamu LHRC |
Wamesema kuwa kutokana
na hayo mtoto wa kitanzania ameendelea kuwa chini huku akikosa haki zake za
msingi huku wizara husika na taasisi husika kushindwa kuwajibika ipasavyo
kuhakikisha mtoto anapata haki zake kwa mujibu wa sheria.
Mkurugenzi mtendaji wa LHRC Mama HELLEN KIJO BISIMBA akizungumzia siku hiyo ya mtoto wa Africa |
Aidha watoto hao
wameishauri serikali kuhakikisha kuwa wanatoa elimu ya haki za mtoto kwa umma
jam,bo ambalo wamesema kuwa litasaidia katika kukuza uelewa wa jamii kuhusu
haki za mtoto wa kitanzania.
No comments:
Post a Comment