Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakia Bilal, akimfariji mke wa aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, Bi Makaje Goso, wakati alipofika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuifariji familia hiyo kabla ya kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea nyumbani kwake Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya maziko yanayotarajia kufanyika leo jioni. Kushoto ni Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Picha na OMR
|
No comments:
Post a Comment