Waziri wa Uchukuzi Samweli Sitta akionesha fomu ya kugombea urais mara katika ukumbi wa NEC makao makauu Dodoma.
Waziri wa Uchukuzi Mh. Samweli Sitta akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fomu leo.
Waziri wa Uchukuzi Mh. Samweli Sitta leo amechukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi makao makuu ya CCM yaliyopo White House Dodoma mjini. Sitta ameambatana na Mke wake pamoja na wapambe wake.
Akizungumza mara baada ya kupokea fomu Sitta amesema kwamba anaomba miaka mitano tu sio zaidi ili aweze kuwashughulikia ipasavyo mafisadi na kumaliza kabisa tatizo la ufisadi unao onekana kukwamisha maendeleo ya ya nchi Hivisasa.
Aidha, ametaja vipaumbele vyake kuwa ni;
(i) Kuulinda muungano
(ii) Kumalizia mchakato wa katiba Pendekezwa
(iii) Kumaliza kabisa suala la Rushwa
(iv) Kuleta mahusiano mazuri kati ya Wafanyabiashara na Serikali
(v) Kuimarisha Chama kiuchumi.
No comments:
Post a Comment