POLISI WAKAMATA BUNDUKI SMG NA JUMLA YA RISASI 59
PAMOJA NA WATUHUMIWA KATIKA MATUKIO TOFAUTI JIJINI DAR ES SALAAM.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uhalifu ikiwa
ni pamoja na unyang’anyi wa kutumia silaha. Watuhumiwa wamekamakwa katika
matukio tofauti jijini Dar es Salaam kufuatia oparesheni kali inayoendelea ya
kuwasaka wahalifu wa makosa mbalimbali.
Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 03/06/2015 majira saa 08:00HRS maeneo ya Tabata Kinyerezi mtaa wa Kibaga
askari wa kikosi kazi (TASK FORCE) walimkamata mtuhumiwa HEMED S/O HASSAN MRISHO @ BUDA, Miaka 31, Mfanyabiashara,
Mkazi wa Tabata Kinyerezi, akiwa na Bunduki aina ya SMG iliyofutwa namba zake
ikiwa na risasi 10. Mtuhumiwa alikamatwa kufuatia taarifa toka kwa msiri kuwa
anajihusisha na uhalifu wa kutumia silaha. Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa
mtuhumiwa HEMED S/O HASSANI akishirikiana na wenzake ambao wanasakwa,
wanajihusisha na unalifu wa kutumia silaha. Atafikishwa mahakamani mara
uchunguzi utakapokamilika.
Katika tukio lingine, mnamo tarehe 01/06/2015 majira ya saa 02:00 huko
maeneo ya Tegeta Mashimo ya Kokoto, Polisi walifanikiwa kukamata risasi 49 za
bunduki aina ya Short Gun zikiwa katika mfuko wa Rambo baada ya kuwakurupua
vijana wanaokaa katika vijiwe vya mashimoni hayo.
Hii ni kufuatia kundi la vijana wanaokadiriwa kufikia kumi wakiwa na mapanga
na silaha nyingine za jadi kuvamia nyumba ya VERONICA D/O SABATH MAMBOYA na
kuiba vitu mbalimbali vikiwemo vitambulisho, TV, Laptop na Pesa taslim TSHS.
300,000/=. Baada ya tukio mlalamikaji alitoa taarifa kituo cha polisi Kawe na
ufuatiliaji ulianza mara moja. Polisi walifanikiwa kuwakamata vijana watatu
ambao walionyesha vijiwe vya vijana wenzao.
Wakati polisi wakijiandaa kuwakamata walikurupuka na kukimbia ndipo
polisi walifanya upekuzi wa eneo hili na kufanikiwa kupata risasi hizo zikiwa
katika mfuko wa plastiki maarufu kama “mfuko wa Rambo”. Watuhumiwa waliokamatwa
ni pamoja na
1. RAMADHANI S/O NUHU, Miaka 20, Mkazi wa Kiwangwa.
2. ABED S/O SALUM, Miaka 18, MKAZi wa Kibaoni.
3. HANIF S/O HAMIS, Miaka 19, MKAzi wa Tegeta.
KUKAMATWA KWA ROLA 15 ZA NYAYA ZA UMEME PAMOJA NA
WATUHUMIWA SABA.
Katika hatua nyingine
Jeshi la Polisi Kanda Maalum limefanikiwa kukamata kontena lenye namba
00LU2876031 likiwa na rola 15 za nyaya (zenye thamani ya shilingi 150,000,000/=
milioni mia moja na hamsini) zilizoibwa tarehe 26/02/2015 zikiwa zinasafirishwa
kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya mradi wa umeme vijijini (REA). Baada ya
wizi wa kontena hilo kesi ilifunguliwa kituo cha Polisi Buguruni na watuhumiwa
watano walikamatwa na kufikishwa mahakamani.
Wakati upelelezi ukiendelea ndipo tarehe 25/05/2015 Polisi Buguruni
walipokea taarifa toka kwa msiri kwamba huko maeneo ya Kibamba mtaa wa
Kibwegele wilaya ya Kimara Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kuna kontena limefichwa
katika kiwanda cha kutengeneza matofali.
Askari wa kikosi kazi walifika eneo la tukio na kukuta kontena hilo
lenye namba 00LU2876031 na walimhoji mlinzi wa eneo ili kupata mmiliki wa eneo
na kontena hilo. Ilipofika saa 23:55hrs mmiliki wa eneo hilo aitwaye DONESIA
D/O AIDAN @ KIFYOGA, Miaka 40, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbezi Makabe ambaye ni
mtuhumiwa wa sita.
Taratibu zilipokamilika kontena hilo lilifunguliwa ndipo zilipokutwa
rolla za nyaya zipatazo 15 kati ya 17 zilizokuwepo katika kontena hilo siku
lilipokuwa linasafirishwa. Tarehe 27/05/2015 majira ya saa 00:30hrs maeneo ya
Kimara mwisho alikamatwa mtuhumiwa mwingine wa saba PROSPER S/O MTEI, Miaka 43,
Mfanyabiashara na upelelezi unaendelea
ili aweze kuunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi ya msingi.
KUKAMATWA KWA BASTOLA MOJA NA MAGANDA YA RISASI
Mnamo tarehe 28/05/2015 majira ya saa 23:00hrs
maeneo ya Kiwalani Minazi Mirefu Kata ya Ilala WIlaya ya Ilala jijini Dar es
Salaam, Polisi walifanikiwa kukamata silaha Bastola yenye nambari 05532 pamoja
na maganda mawili ya risasi aina ya SMG katika eneo la tukio baada ya majambazi
kuitelekeza mara walipozingirwa na wananchi waliotaka kuwakamata.
Majambazi hao walikuwa wamefanya tukio la uporaji maeneo ya vingunguti
wakitumia pikipiki mbili ambapo moja ina namba za usajili MC610 ABU aina ya
Boxer rangi nyekundu ambayo pia waliipora kwa mtoa taarifa. Aidha katika tukio
hilo pia majambazi hao walimpiga mtoa taarifa na kitako cha bunduki waliyokuwa
nayo kisha kumpora pikipiki hiyo na pesa taslim shilingi 300,000/= Hata hivyo
majambazi hao walifanikiwa kutoroka. Polisi kwa kushirikiana na wananchi
waliweza kuikamata pikipiki hiyo.
KUKAMATWA KWA VIPANDE 20 VYA PEMBE ZA NDOVU.
Katika oparesheni iliyoendeshwa tarehe 25/05/2015
na idara ya INTERPOL jijini Dar es Salaam ya kukamata magari, madawa ya kulevya
na uhalifu mwingine. Ilipofika majira ya saa 18:00hrs maeneo ya Kimara Suka
ambapo kutokana na foleni ya magari iliyosababishwa na ukaguzi wa magari katika
zoezi hilo alishuka kijana mmoja mwenye umri kati ya miaka 39- 45 kwa dhumuni
la kukodi pikipiki.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida baada ya kuwaona askari wa unifomu
kijana huyo alitupa kifurushi alichokuwa nacho na kukimbia. Askari walilichukua
hilo furushi na kulipekuwa na kukuta kuna meno ya tembo vipande ishirini pamoja
na nguo kuku. Kielelezo kilipelekwa kituo cha Polisi Mbezi na kufunguliwa
jalada la uchunguzi KMR/PE/67/2015.
KUKAMATWA KWA MLIPUKO, VIFAA VYA KUVUNJIA, DAWA ZA
KULEVYA PAMOJA NA MTUHUMIWA.
Tarehe 04/06/2015 majira ya saa 10:00hrs maeneo ya Chamazi ulifanyika
msako mkali wa kupambana na uhalifu na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa MICHAEL
S/O KASAMBALE, Miaka 28, Mkazi wa Chamazi akiwa na mlipuko mmoja na vifaa vya
kuvunjia. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika. Aidha
mtuhumiwa huyo amekamatwa na kete kadhaa za madawa ya kulevya.
KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA AKIWA NA BASTOLA BANDIA
Polisi wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa JACOB S/O NATHANIEL MWETA,
Miaka 30, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kimara ambaye alikuwa anaitumia kutishia
watu kisha kupora. Mtuhumiwa ame kiri kuhusika katika matukio kadhaa ya
unyang’anyi hasa katika maeneo ya Tegeta na Kunduchi jijini Dar es Salaam.
MAFANIKIO MENGINE YA OPARESHENI INAYOENDELEA
JIJINI DAR ES SALAAM.
Aidha, Jeshi la Polisi
Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na oparesheni ya kupambana na uhalifu
katika jiji la Dar es Salaam na kufanikiwa kukamata vitu vifuatavyo:
1. Mitambo mitano (5) ya kutengeneza pombe ya moshi
(Gongo)
2. JUmla ya lita mia mbili (200) za pombe ya Moshi
(Gongo)
3. Gunia mbili za banghi.
4. Kupatikana na Mirungi box moja (1).
5. Kete kadhaa za madawa ya kulevya.
SIMON SIRRO
– DCP
KNY.
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment