Tuesday, June 2, 2015

TIGO YAZINDIUA DUKA MOSHI MJINI,PICHA NA STORY ZOTE ZIKO HAPA

     Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas T. Gama akikata utepe kuzindua rasmi Tawi la Tigo Moshi Mjini jana, wanaoshuhudia kuliani Gwamaka Mwakilembe, Meneja huduma kwa wateja Kanda ya Kaskazini na kushotoni Meneja wa ubora huduma kwa wateja Tigo, Mwangaza Matotola.

     Meneja huduma kwa wateja Kanda ya Kaskazini, Gwamaka Mwakilembe akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas Gama juu ya bidhaa zilizopo ndani ya Duka la Tigo lililozinduliwa Moshi Mjini jana.
   Meneja wa Ubora huduma kwa Wateja Tigo, Mwangaza Matotola akiongea na waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapopichani) wakati wa uzinduzi wa Duka la Tigo Moshi Mjini, wengine kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas Gama na kulia Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Novatus makunga.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas T. Gama akiongea na waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapopichani) wakati wa uzinduzi wa Tawi la Tigo Moshi Mjini jana, wengine kulia Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Novatus Makunga na kushoto Meneja wa Ubora huduma kwa Wateja Tigo, Mwanga za Matotola

Meneja  wa Mawasiliano Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa Duka la Tigo moshi Mjini.

   Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Novatus Makunga akiongea na wageni waalikwa wakati wauzinduzi wa Tawi la Tigo Moshi Mjini, wengine kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe. Leonidas Gama, Katibu wa Mkuu waMkoa Daniel Mchomvu na kulia ni Meneja wa ubora hudma kwa Wateja Tigo, Mwangaza Matotola

   Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuiniya Tigo wakimsikiliza mgeni rasmi Mhe. Leonnidas Gama wakati wa uzinduzi wa Duka la Tigo moshi Mjini.

Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe. Leonidas Gama (kulia), Mwangaza Matotola Meneja wa Ubora huduma kwa Wateja Tigo (katikati) na Meneja wa Mawasiliano Tigo, John Wanyancha (kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, leo imezindua duka jipya la kuhudumia wateja mjini Moshi, duka hilo jipya limefunguliwa ili kuwaondolea usumbufu wateja wa Tigo ambao walikuwa wakisubiria huduma kwa muda mrefu katika duka moja lililokuwapo mjini humo.

Akiongea wakati wa ufunguzi, Meneja wa Ubora wa Huduma kwa Wateja Mwangaza Matotola alisema duka hilo jipya litasaidia kupunguza msongamano katika duka la awali na pia limejengwa ili kutimiza malengo ya kampuni ya kutanua wigo wa huduma zake.

“Tigo ni kampuni ambayo inawajali sana wateja wake, na kwa sababu hii tuliamua kufungua duka jingine ambalo mbali ya kuwahudumia wateja wetu kwa haraka pia litasogeza huduma karibu zaidi na wateja wetu,” alisema Mwangaza.

Uzinduzi wa duka hilo umefanyika ikiwa ni siku moja tu baada ya kampuni ya Tigo kufungua duka lilokarabatiwa jijini Arusha, maduka haya yana lengo la kuboresha na kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

Kwa mujibu wa Mwangaza, duka hilo ambalo limejengwa katika Mtaa wa Rengua linategemewa kuhudumia wateja 250 kwa siku likitoa huduma mbalimbali za Tigo ikiwamo intaneti, kadi za simu, muda wa hewani, huduma za namba na pia huduma za kifedha.

“Duka hili ni la muhimu sana katika kuhudumia wateja wetu, kwa sababu eneo lilipo ni karibu na wananchi, hii itawezesha upatikanaji wa huduma kwa haraka zaidi,” alisema Diego huku akiongeza kuwa duka hilo pia litahudumia wakaazi wa vitongoji na wilaya za jirani kama Uru, Kibosho, Marangu, Bomang’ombe na Hai.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini David Charles alisema Tigo ni kampuni ambayo inathamini maendeleo ya nchi, na kwa hilo inajitahidi kuwaondolea wanachi adha ya kutumia muda mrefu wakitfuta huduma na badala yake wautumie muda huo kufanya shughuli mbalimbali za kujenga taifa.

Kwa mujibu wa Mwangaza, duka jipya la mjini Moshi linafanya idadi ya maduka ya kampuni ya Tigo kuwa (xx) na huku kukiwa na mipango ya kufungua maduka mengi zaidi nchini.



No comments: