1.Niko mbele yenu sio kufanya kampeni ya urais, niko mbele yenu kuomba ridhaa ya yenu kugombea nafasi ya urais muda ukifika.
2. Siko hapa kumlaumu mtu au ukimshambulia kwa sababu ukimlaumu mtu umAsikini bado uko palepale. Nikisema historia yangu yote muda hautatosha, kisomo nimesoma mpaka mwisho wa kusoma, kama ni taalumu nimefikia mwisho.
3.Nimepata bahati ya kusoma vyuo vikubwa sana duniani na sehemu kubwa nimepatia Ujerumani ndio maana wengine wanasema nafanya kazi kijerumani.
4. Nimefanya utafiti kwa miaka 30,chama cha majiologia wamerekani kilichoanza mwaka 1988, mimi niko ngazi ya juu pia kwa waingereza na wachina niko ngazi ya juu kabisa.
5.Kwenye uasisi mwaka 1976, CCM inaanza 77 sisi ndo waasisi, kadi hii hapa. Kama nimeweza kutunza kadi ya CCM tangu 75 basi mimi ndio naweza kutunza rasilimali zenu.
6.Toka tunapata uhuru tuna vikwazo, ujinga, maradhi na umasikini Mwl alitueleza. Nil lazima matatizo yatakuwepo kwenye jamii.
7.Rushwa kubwa na ndogo, ukosefu wa ajira, siasa imekwenda kila mahala, taifa linanyemelewa na uvuvu na utegemezi, dhulma, upungufu wa upatikanaji wa takwimu sahihi, tumepungukiwa ushindani kama taifa, tumeshindwa kujiamini.
8. Haya ndio nataka kuyashughulikia mimi. Upungufu wa mshikamano wa taifa letu. Kwetu asilimia 51 waislamu na 49 wakristo hivyo matatizo ya madhehebu hapa ndipo mahala pake. Afrika ina nchi 54, mimi nimeeenda 52 kasoro Mauritania na Chad. Ningekua sio muaminifu nisingepokelewa huko, ulaya nimezunguka.
9.Lazima Tujue hali halisi ya uchumi wetu, chukueni kalamu na karatasi. Lazima useme unatoka wapi unaenda wapi! India asilimia 74 wanajua kusoma na kuandika. Nchi inayoongoza kwa watafiti ni Finland.(Anataja takwimu za nchi ambazo tulikuwa tunafanana uchumi baada ya vita ya pili ya dunia ikiwemo India, Brazil, China na Kenya.) Sipendi sana kujilinganisha na Kenya kwa sababu sote ni maskini.
10.Dira ya maendeleo inasema miaka kumi kutoka sasa Tanzania isiwe nchi masikini, tusikae pembeni, tusogee juu kidogo. Hakuna mwenye uwezo huo ni mimi tu ili tufikie pato la dola bilioni 200 kutoka dila bilioni 40. Mwaka 2025 tutakuwa milioni 60, nataka tule miogo na viazi kwa hamu na sio kwa shida.
11.Siwezi kukupa ahadi ya mishahara wakati sijakuza uchumi, siwezi kukupa ahadi ya kukujengea shule wakati sijakuza uchumi, tukuze kwanza uchumi. |
No comments:
Post a Comment