Saturday, June 13, 2015

WASOMI WA SAIKOLOJIA KUTOKA UDSM WATOA ELIMU KWA WATOTO WA SOS CHILIDRENS VILLAGE JIJINI DAR ES SALAAM

Wanafunzi wanaosoma masomo ya PSYCHOLOGIA  kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM jana wameendesha semina ama mafunzo maalumkwa watoto wanaoishi katika Kituo cha kulea watoto wenye uhitaji maalum cha SOS CHILDRENS VILLAGE kilichopo ubungo Jijini Dar es Salaam karibu na kituo cha mabasi cha mawasiliano,mafunzo yaliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo wanafuzi hao wa kujitambua,kujiamini,kujikubali na kutambua uwezo wao kama watoto wa Kitanzania.

Mtandao huu ulipita katika kituo hicho na kushuhudia mamia ya watoto wa kituo hicho wakifurahia mafunzo hayo ambayo yalielezwa kama moja ya mambo muhimu wanayotakiwa kupewa watoto hao kwa ajili ya malezi kulingana na mazingira wanayoishi.
Akizngumza na mtandao huu mmoja wa wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam JOSEPHAT SHAMI ambaye ni mwanafuzi wa mwaka wa tatu na ambaye ni mmoja wa wanachama wa chama cha wanafuzi wa kitivo cha saikologia alisema kuwa mafunzo hayo ni muendelezo wa mafunzo ambayo wamekuwa wakiyatoka katika maeneo mbalimbali ambayo kuna wahitaji kama hao wakiwemo watoto,wanafunzi,watumiaji wa madawa ya kulevya  pamoja na wazee mbalimbali.
Alisema kuwa inawasukuma kufanya hivyo kwani ni ukweli kuwa matatizo ya kisaikologia hasa kwa watoto yamekuwa yakiathiri ustawi mzuri wa watoto hasa watoto wanaoishi katika mazingira magumu jambo ambalo wamesema kuwa limewasukuma kufanya mafuzo hayo kuwajenga kisaikoligia makundi hayo maalumu ili waweze kufikisha ndoto zao kimaisha.

Tulipata nafasi ya kuzungumza na mmoja  wa walezi wa kituo hicho ambacho kulikuwa kunaendelea mafunzo hayo ambaye alijitambulisha kwa jina la LEAH MTALAI  alitueleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa watoto hao kwani yatawasaidia kujijenga kitabia na kufikra na kutambua kuwa wana uwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa sana ukilinganisha na jinsi wanavyojichukulia,ambapo amesema kuwa kutembelewa na wanafuzi hao kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam kwa ajili ya mafunzo hayo ni bahati ya aina yake na inatakiwa kuigwa na watu mbalimbali kutoka taaluma tofauti kuzitumia taaluma zao kuijenga jamii yenye ustawi na mwisho watakuwa wamelisaidia taifa kwa ujumla

Wanafunzi kutoka UDSM taaluma ya saikologia wakifwatilia mafunzo hayo yaliyokuwa yanaendelea katika kituo cha kulelea watoto cha SOS CHILDRENS VILLAGE kilichopo Jijini Dar es saalaam

No comments: