Mkuu wilaya ya Temeke Sophia Mjema amewapongeza
madiwani wa manispaa ya temeke kwa kutekeleza ahadi zao kwa wananchi kwa zaidi
ya asilimia 90.
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo wakati wa shughuli ya
kufunga rasmi baraza la madiwani Temeke amesema kuwa asilimia kubwa ya miradi
mbalimbali katika manispaa hiyo imekamilika kwa asilimia kubwa kutokana na
ushirikiano mzuri wa viongozi na madiwani hao,ikiwemo shule,maabara,hospitali,huku
akisema kuwa angependa kuwaona madiwani hao wakirejea katika nyazifa hizo hata
baada ya uchaguzi mkuu na kuendelea kuifanya manispaa hiyo kuwa bora katika manispaa
zote nchini.
Aidha akizngumza katika mkutano huo meya wa Temeke
MAABAD HOJA amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano wamefanikiwa kukusanya
mapato kwa zaidi ya asilima 90,na kufanikiwa kupata hati safi kutokana na kuwa
na viongozi bora na wenye kufwata maadili.
Aidha meya
huyo amelivunja rasmi baraza hilo la madiwani huku akiowataka kuendelea
kufanya kazi za kuwasaidia wananchi wakati wakiendelea kuomba ridhaa ya
wananchi ili waweze kurejea tena katika nafasi zao.
PICHA CHINI NI MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MKUTANO HUO
|
No comments:
Post a Comment