Waumini wa Dini ya Kislam
pamoja na wakristo nchini Tanzania pamoja wapenda amani wote Tanzania na duniani leo
wameungana na wapinga dhuluma nchini kote katikamatembezi ya aman ya kulaani
dhuluma na uonevu mbalimbali wanaofanyiwa wanaadamu hususani mauaji
yanayoendelea nchini palestina.
Matembezi hayo ya amani
yamefanyika asubuhi ya leo Jijini Dar es salaam ya kuanzia msikiti wa
kichangani uliopo magomeni jijini dare s salaam hadi kufika kigogo ambapo
yamehudhuriwa na viongozi na waumini wa dini mbalimbali nchini Tanzania lengo
likiwa ni kupinga unyanyasaji wanaofanyiwa wanadamu nchini palestina na mataifa
mengine ambayo unyama huo unafanyika.
Katika matembezi hayo
mtandao huu ulipata nafasi ya kuhudhuria ambapo mwandishi wetu alizungumza na
kiongozi mkuu wa waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Shekh HEMED
JALALA ambaye amesema kuwa waumini wa dini pamoja na viongozi mbalimbali katika
nchi ya Tanzania wanatakiwa kuliangalia taifa la palestina kwa jicho la tatu
kama wanavyoliangalia taifa la Tanzania kutokana na kutengwa na mataifa mengine
huku wananchi wa taifa hilo wakiendelea kuteseka kutokana na vita vilivyodumu
kwa muda mrefu sasa takribani miaka 67 .
Ameongeza kuwa kwa sasa
ni wajibu wa kila kiongozi wa dini na wapinga dhuluma kote nchini kuhakikisha
kuwa wanaueleza ulimwengu juu ya kile ambacho kinaendelea katika mataifa hayo
ikiwemo taifa la palestina na kuwaeleza watu juu ya umuhimu wa taifa la
palestina na Tanzania kwa dunia na historia yake kwa ujumla.
Amesema kuwa haki
yoyote wanayodhulumiwa wapalestina haki hiyo wamedhulumiwa watanzania waislam na wakristo na unyanganyi wowote wa
ardhi wanaofanyiwa wapalestina haujafanywa kwa waislam tuu bali umefanywa kwa
madhehebu na dini zote duniani hivyo ni lazima dunia iungane kuwatetea
wapelestina hao
Maadhimisho hayo
yamefanyika ikiwa leo siku ya kimataifa ya QUDS ambayo ni siku ya ukombozi wa
mwanadamu duniani kutoka katika uonevu,ukandamizaji,na unyanyasaji wa mwanadamu
ambapo palestina ndio msikiti wa QUDS unakopatikana
Matembezi hayo
yamewakutanisha waislam na wakristo pamoja na wapenda amani duniani kote
yamefanyika leo Jijini Dar es salaam ikiwa ni ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu
wa Ramadhan ambayo yameandaliwa na HAWZAT IMAM SWADIQ,pamoja na kamati ya Quds
na Tanzania Itnasheriya Community(T.I.C).
PICHA NYINGINE NYINGI ZA TUKIO HILO ZIPO CHINI
No comments:
Post a Comment