Baadhi ya madiwani kama wanavyoonekana katika picha ambao wametoka katika vyama vya UDP na CCM katika wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wameamua kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Akiwataja majina madiwani hao Katibu Mwenezi Chadema wilayani Bariadi Martine Mogani, alisema kuwa kati ya hao, watatu ni kutoka CCM na saba kutoka UDP ambao ni Benjamini Matondo (UDP) Nyakabindi, Shiwa Danhi (UDP) Sapiwi na Gulya Nyembe (UDP) Ihusi.
Mtia nia nafasi ya Ubunge katika jimbo la Bariadi Magharibi Seni Silanga kupitia Chadema, akiongea na mamia ya wananchi katika kata ya Dutwa wakati wa kutambulishwa kwa madiwani 10 waliojiunga na chama hicho.
Watia nia nafasi ya ubunge jimbo la Bariadi Magharibi kupitia Chadema.
Mgombea nafasi ya ubunge Godwin Simba kupitia Chadema akiongea na wananchi wa kata ya Dutwa.
No comments:
Post a Comment