Tuesday, August 4, 2015

JUKATA WAKUMBUSHIA KATIBA MPYA

Makamu mweyekiti wa JUKATA ndugu HEBRON MWAKAGENDA akizngumza na wanahabari asubuhi ya leo
Jukawaa la katiba nchini Tanzania JUKATA leo limetoa wito kwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dk JAKAYA MRISHO KIKWETE kutoa kauli rasmi juu ya uendelezwaji wa mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya kutokana na kile walichosema mchakato huo umeahirishwa kienyeji na kuwaacha watanzania njia panda.

Akizungumza na wananhabari mapama leo makamu mweyekiti wa JUKATA ndugu HEBRON MWAKAGENDA amesema kuwa ni wazi kuwa serikali imeshindwa kuwapatia watanzania katiba mpya kwa kipindi walichoahidiwa na sasa mchakato huo umeahirishwa kimya kimya jambo ambalo amesema lazima watanzania wapewe taarifa rasmi juu ya mchakato huo.

Ndugu Mwakagenda amesema kuwa swala la Katiba mpya kwa watanzania ni jambolenye maslahi mapana kwa taifa na kama rais wa Tanzania lazima aonyeshe nia ya kuendeleza mchakato wa upatikanaji wa katiba na ni lazima atoe taariufa rasmi ya mchakato huo ili watanzania wasibaki na maswali kuhusu swala hilo.
 

Aidha ameongeza kuwa kwa kuwa nchi inaendelea katika uchaguzi mkuu wa kumpata kiongozi mpya wa taifa hili ni lazima rais ajeye ahakikishe kuwa anaitoisha mkutano mkuu wa katiba ambao utawakutanisha wadau mbalimbali wa maswala ya katiba kwa lengo la kujadili mstakabali wa katiba mpya  kwa kuwa sasa mchakato huo umeonekana kukwama kupatikana kwa katiba mpya.

No comments: