Tuesday, August 4, 2015

ADC watoa ya moyoni juu ya usajili wa kisiasa unaoendelea nchini

Mwenyekiti wa Chama cha ADC Mhe. Said Miraj Akisalimiana na mlezi wa chama hicho ambaye sasa ndiye mgombea wa urais zanzibar  kwa tiketi ya chama hicho wakisalimiana wakati wa ufumnguzi wa mkutano huo
 Wakati macho na maskio ya watania yakiwa yanaangalia mnyukano wa kisiasa unaoendelea nchini baina ya chama cha mapinduzi na umoja wa katiba ya wananchi UKAWA nacho chama kipya kinachokuja kwa kasi chama cha ADC wameibuka na kusema kitendo kilichofanywa na vyama vya upinzani kuwachukua baadhi ya viongozi wa chama tawala na kuwapa madaraka ni muendelezo wa kuwasaliti watanzania na kuendelea kuipa nafasi CCM .
Mwenyekiti wa Chama cha ADC Mhe. Said Miraj akizngumza na wajumbe wa mkutano huo
Akizngumza wakati akifungua mkutano mkuu wa bodi ya wanachama wanaokutana jijini Dar es salaam kwa lengo la kupitisha majina ya wagombea urais wa chama hicho,mwenyekiti wa chama hicho  cha ADC Mhe. Said Mirajamesema kuwa kwa hali ilivyo sasa uchaguzi unaokuja mwezi wa kumi utakuwa kati ya ccm na ccm wenyewe huku upinzani ukiwa hauna nguvu kutokana na kuwapikea baadhi ya makada wa chama chama mapinduzi na kuwapa dhamana kubwa ndani ya vyama hivyo.
Wajumbe wakiwa katika mkutano huo
Amesema kuwa kwa hali inayoendelea sasa nchini Tanzania ni wazi kuwa hakuna mtanzania aliye na nia ya dhati ya kuwasaidia watanzania ila ni ADC pekee kwa kuwa wao hawako tayari kuwapokea makada wa chama chochote waliokatwa na kuwapa madaraka kwani nao ndio wanaweza kuwarudisha watanzania tena kule ambapo wanakupinga.

Kauli hii inakuja ikiwa waziri mkuu wa zamani wa Tanzania mh EDWARD LOWASA amekihama chama chake na kuhamia cha cha democrasia na maendeleo chadema huku makada kadhaa wa chama hicho wakiendelea kukihama chama hicho na kujiunga na vyama vya upinzani.



No comments: