Wakati mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania ikiendelea kufanya juhudi za kutatua tatizo hili, safari zetu za usiku za kuingia na kutoka jijini Mwanza zinaendelea kusitishwa na tutawapa maelezo zaidi mapema iwezekavyo huduma zetu zitakaporejea.
Tunawataarifu kuwa safari zetu za mchana zinaendelea kikamilifu na wateja wa Fastjet wana haki ya kuahirisha safari zao zilizositishwa au kupata tiketi nyingine ndani ya siku saba kuanzia leo au kudai pesa kwa tiketi zozote ambazo hazikutumika.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kwamba, usalama wao ndio wajibu wetu mkubwa!
Habari zaidi zitakuwa zikitolewa pale zinapopatikana.
No comments:
Post a Comment