Monday, August 3, 2015

Maamuzi magumu ya CHADEMA muda huu kuhusu Dk SLAA,Soma hapa

Mwenyekiti wa chama cha Democrasia maendeleo chadema FREMAN MBOWE akizngumza na wajumbe wa baraza kuu katika mkutano unaoendelea jijini Dar es salaam leo
 Chama cha democrasia na maendleo CHADEMA kimetangaza rasmi kumruhusu Katibu Mkuu wa chama hicho Dk WILBROD SLAA kuchukua muda wa kupumzika akitafakari uwepo wake ndani ya chama hicho kutokana na yeye kutokukubaliana na maaamuuzi ya kumpokea wziri mkuu wa zaman ndugu EDWARD LOWASA.
Akizungumza na wajumbe wa Baraza kuu la chama hicho wakati wa ufunguzi wa mkutano wa baraza hilo mwenyekiti wa chama hicho MH FREMAN MBOWE amesema kuwa chama hicho hakina mgogoro wala ugomvi wowote na katibu mkuu wake kama inavyoelezwa na baadhi ya mitandao bali kinachoendelea ni mchakato wa kidemocrasia wa kukubaliana na kutafakari maamuzi ya kamati kuu ya chama hicho.
Wajumbe wakishangilia baada ya mwenyekiti huyo kutangaza maamuzi juu ya katibu mkuu wa chama hicho DK WILBROD SLAA
Amesema kuwa mchakato wa kumchukua EDWARD LOWASA ulipitia katika ngazi zote za vikao ambavyo pia katibu mkuu dk SLAA alikuwepo ila kilichotokea ni kutofautiana kwa mawazo mwishoni mwa mchakato huo jambo ambalo amesema haliwezi kuwarudisha nyuma kwani muda hausubiri na uchaguzi mkuu unakaribia.

Ameongeza kuwa amekuwa na vikao vingi na dk SLAA tangu kutokea kwa mkanganyiko huo vikao ambavyo wamekubaliana kumpa muda kiongozi huyo kutafakari juu ya uwepo wake ndani ya harakati za kuingoa CCM madarakani wakati chama kinasonga mbele na akishafanya maamuzi ataungana na chama hicho muda na siku yoyote.

Kumekuwa na taarifa zinazotoka katika magazeti kadhaa zinazoeleza kuwa dk SLAA tayari ameshaandika barua ya kuacha kazi na amerudisha vifaa vyote vya chama jambo ambalo mwenyekiti huyo amelipinga na kusema kuwa maneno hayo ni vita inayoendelea baina ya chama hicho dhidi ya wapinzani wake.

Aidha katika hatua iliyokuwa haitarajiwi mwenyekiti huyo aliwahoji wajumbe wote waliokuwa kwenye kikao hicho kama wanakubaliana kumpumzisha Dk SLAA kwa muda huku harakati za kujiandaa na uchaguzi zikiendelea ambapo wajumbe wote walisimama na kushangilia ishara ya kukubaliana na maamuzi ya chama hicho ambapo wengi wamekuwa na imani kuwa Dk SLAA atarejea na kujiunga tena na chama hicho

No comments: