Kamanda Mpinga, akishiriki dua ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini, baada ya mazoezi yao timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki na timu ya Kamati ya Amani ya Mkoa wa Arusha unaotarajia kuchezwa mwezi ujao jijini Arusha na ule wa kirafiki kati yao na timu ya Mabalozi hivi karibuni. Kamanda Mpinga alifika kuwatembelea wachezaji hao kujionea maendeleo ya mazoezi yao. |
Kamanda Mpiga akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini ya Mkoa wa Dar es Salaam,baada ya mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo asubuhi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Kamanda Mpinga alifika kuwatembelea wachezaji hao kujionea maendeleo ya mazoezi yao. |
5:- Kamanda Mpinga, akisalimiana na walimu wa timu hiyo, baada ya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi. |
6 hadi 10:- Kamanda Mpinga akisalimiana na wachezaji wa timu hiyo baada ya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
Mchungaji wa Kanisa la Penuel Healing Ministry Ubungo Kibangu, Mch. Alphonce Temba (kulia) akimramba chenga Mchungaji wa Kanisa la KKKT Mashariki ya Pwania, George Fupe, wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi kwa ajili ya kujiandaa na michezo kadhaa ya kirafiki kwa ajili ya kuimarisha amani na mshikamano kwa watanzania.
Ustaadh Sale (katikati) akimiliki mpira katikati ya mabeki wa timu pinzani, wakati wa mazoezi ya timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa dini yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi kwa ajili ya kujiandaa na michezo kadhaa ya kirafiki kwa ajili ya kuimarisha amani na mshikamano kwa watanzania.
Picha ma www.sufianimafoto.com
No comments:
Post a Comment