Umoja wa katiba ya
wananchi UKAWA umesisitiza kuwa utazindua kampeni zake siku ya jumamosi ya
tarehe 29 mwezi huu katika viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam licha ya
mizengwe wanayowekewa na mansipaa ya ilala ya kuwanyima kutumia uwanja huo kwa
sababu ya kuwa na matumizi mengine siku hiyo.
Akizunzgumza na
wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa NCCR mageuzi ambaye
pia ni mwenyekiti mwenza wa umoja huo JAMES MBATIA amesema kuwa uzinduzi huo
utafanyika siku ya jumamosi kama ilivyopangwa japo manispaa ya ilala
imewaandikia barua ya kuwa na matumizi
mengine siku hiyo.
Mbatia amesema kuwa
wamepeka maombi ya kutumia uwanja huo na wamejibiwa kuwa kuna watu
wameshauchukua kwa ajili ya kazi nyingine ambapo walipojaribu kuuliza ni mtu
gani ili wazungumze naye manispaa hiyo imegoma kumtaja na kusisitiza kuwa
uwanja huo utakuwa ukitumika siku hiyo ya jumamosi.
Mbatia amesema kuwa
kumekua na mbinu chafu ambazo zinatumiwa na serikali kupitia wakuu wa mikoa na
wakuu wa wilaya za kuhujumu harakati za kampeni za umoja huo lakini wamejipanga
kuhakikisha kuwa wanatetea haki yao na kuleta usawa katika kampeni hizo.
Akitolea mfano wa
mgombea EDWARD LOWASA leo kunyimwa kuendelea na ziara yake ambayo leo ilipangwa
kufanyika katika baadhi ya hospiytali kuzungumza na wagonjwa huku mgombea
mwenza wa chama cha mapinduzi SAMIA SULUHU akiendelea na zoezi kama hilo mkoani
kilimanjario jambo ambalo amesema kuwa ni rafu ya wazi ambayo kamwe hawawezi
kuivumilia.
Akizungumzia swala la
kampeni ya chama cha mapinduzi siku ya uzinduzi kufanyika hadi saa kumi na
mbili na nusu kinyume na sheria za uchaguzi mbatia amesema kuwa tume ya taifa
ya uchaguzi imekuwa ikikaa kimya kwa kuwa kitendo hicho kilifanywa na chama tawala
lakini kingefanyika na chama cha upinzani lazima wangepigwa mabomu jambo ambalo
amedai kuwa ni kuendelea kuwajaza hasira watanzania ambao wengi sasa wamekuwa
na kiu ya mabadiliko nchini.
No comments:
Post a Comment